The House of Favourite Newspapers

Mkazi wa Mwanza Ajishindia Mil 20 za Promosheni ya Vodacom

0

001.KAMATA MPUNGA

Meneja Uendelezaji wa Masuala ya Kibiashara wa Vodacom Tanzania (Business Continuity Management), Ajit Mistry (kushoto) na Afisa msimamizi wa michezo ya kubahatisha Tanzania, Abdallah Hamed (wa pili kushoto) wakimshuhudia Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia) akiwaonyesha namba ya simu ya Shomari Almasi mkazi wa Mwanza aliyeibuka mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 20/- katika droo ya mwezi ya promosheni ya ‘Kamata Mpunga’ inayowawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia pesa taslimu kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100. Jumla ya washindi 61 wamepatikana kupitia promosheni hiyo. Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO” kwenda namba 15544 aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neno ”WIN” kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali.
002.KAMATA MPUNGA
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuchezesha droo ya mwezi ya promosheni ya”Kamata Mpunga”ambapo Shomari Almasi, mkazi wa Mwanza, aliibuka mshindi wa mwezi wa kitita cha shilingi Milioni 20/- Wengine katika picha kushoto ni Ofisa msimamizi wa michezo ya kubahatisha Tanzania, Abdallah Hamed na Meneja wa huduma za ziada wa kampuni hiyo, Mathew Kampambe.

Mkazi wa kitongoji cha Mkoani kilichopo Nyamagana jijini Mwanza,Shomari Almas ameibuka mshindi mwezi wa kitita cha shilingi milioni 20 kupitia promosheni ya ”Kamata Mpunga”inayoendeshwa na Vodacom Tanzania.

Akiongea kwa furaha baada ya kutangazwa kuwa ameibuka kuwa mshindi wa droo ya mwezi Shomari Almasi ambaye anajishughulisha na kilimo na ufugaji alisema kuwa ndoto yake ya kuboresha maisha yake imetimia.

“Nashukuru Vodacom kwa kuleta promosheni hii kwa kuwa wakati nashiriki sikujua kama nitaibuka na ushindi.Nikipatiwa fedha hizo nitaendeleza shughuli zangu za kilimo na ufugaji pia mipango yangu ya kuoa na kuazisha familia yangu itafanikiwa”.Alisema.

Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amesema kuwa promosheni hii ambayo inaendelea imeishawezesha wateja 61 wa Vodacom kujishindia vitita vya mamilioni ya fedha.Washindi 58 wamejinyakulia shilingi milioni 1 kila mmoja,washindi watatu wa mwezi wamejinyakulia shilingi milioni 5 kila mmoja.

“Napenda kutoa wito kwa wateja wetu na watanzania wote kwa ujumla ambao hawajajiunga na mtandao wetu waweze kujiunga na kuchangamkia promosheni hii kwani kila siku kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi kuna washindi 3 ambapo kila mshindi anajinyakulia shilingi Milioni 1/- na kila mwisho wa wiki yaani Jumapili kuna mshindi mmoja wa Milioni 5/= na mwisho wa mwezi kuna mshindi wa milioni 20/= na kuna mshindi wa zawadi kubwa ya mwisho wa promosheni ni ya kitita cha shilingi Milioni 100/= “Alisema

Aliongeza kusema kuwa ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii ni rahisi sana mteja anachotakiwa kufanya ni kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa kuandika neno “GO” kwenda namba 15544 ambapo atapata ujumbe wa kumfahamisha kuwa ameingia kwenye mchezo na ataanza kupokea maswali atakayotakiwa kuyajibu kwa ajili ya kujiongezea pointi za ushindi na mteja atakatwa shilingi 300 tu kwenye muda wake wa maongezi ”. maswali atakayopokea mteja yatakuwa na majibu 2 moja likiwa jibu sahihi na lingine likiwa sio sahihi.

Kwa wateja ambao hawana nafasi ya kujibu maswali ili wasipitwe na promosheni hii alisema wanatakiwa kutuma neno “WIN” kwenda namba 15544 na atakatwa kiasi cha shilingi 200 tu watakuwa hawahangaiki kujibu maswali ila watakuwa wameingizwa kwa droo moja kwa moja.

Leave A Reply