The House of Favourite Newspapers

Mke Ampa Majukumu Mazito Fiston Yanga

0

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Abdoul Razack amefunguka kuwa kabla hajatua kikosini hapo, alipewa masharti mazito na mkewe ya kuhakikisha anafanya vizuri ndani ya timu hiyo ikiwemo kufunga mabao mengi kama ambavyo alikuwa akifanya katika timu ya taifa ya Burundi.

 

Fiston ni usajili mpya ndani ya Yanga uliosajiliwa katika dirisha dogo kwa ajili ya kuboresha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Fiston alisema kuwa wakati anaondoka Burundi kuja Tanzania, mkewe alimuaga kwa kumuambia ahakikishe anafanya vizuri akiwa Yanga ikiwezekana kufunga mabao ambayo yataisadia timu kama ambavyo alikuwa akifanya katika kikosi cha timu ya taifa ya Burundi.

 

“Wakati naondoka nchini Burundi kuja Tanzania mke wangu aliniaga kwa kuniambia nikapambane ndani Yanga kama ambavyo napambana nikiwa na timu ya taifa, aliniambia natakiwa kufunga mabao mengi kwani nikifanya hivyo ndani ya Yanga nitazidi kujitangaza kutokana na umaarufu mkubwa wa klabu hiyo.“

 

Hivyo maneno ya mke wangu nayazingatia na naahidi nitajitahidi kufanya kama ambavyo aliniambia, nitafunga mabao mengi kuisaidia timu yangu kubaki nafasi ya kwanza msimu huu na nipo tayari kufia uwanjani lakini timu iweze kusalia nafasi ya kwanza hatimaye kutwaa ubingwa,” alisema mshambuliaji huyo.

STORI: MARCO NZUMBE, Dar es Salaam

Leave A Reply