The House of Favourite Newspapers

MKE NUSURA ABAKWE NA SANGOMA

Hii inatisha! Mganga wa kienyeji aliyetambulika kwa jina moja la Luiza, hivi karibuni alinaswa chumbani kwa mke wa mtu akidaiwa kuwa alikuwa na dhamira ya kumbaka kwa maelezo kwamba ndiyo njia anayotumia katika kuwatibu watu wenye matatizo ya kutonasa ujauzito.

 

Tukio hilo lililostaajabisha wengi lilijiri juzi, Alhamisi maeneo ya Mabibo jijini Dar ambapo ilidaiwa kuwa, sangoma huyo alimrubuni mama huyo kuwa, kama anataka dawa ya kupata mimba, anayo, lakini ni ya aina yake.

MSIKIE SHUHUDA

Akizungumza na Risasi Jumamosi, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina la Hamisa Kisaki alisema:

“Sisi bwana tulishangaa kuona Polisi wanavamia kwenye chumba cha huyu mwanamke na baadaye tukagundua kumbe walikuwa wamekuja kumnasa sangoma huyo kwa madai kuwa amekuwa akitapeli watu kwamba anatoa dawa ya ujauzito, lakini kumbe hana lolote.”

MKE ASIMULIA TUKIO ZIMA

Akisimulia mkasa ulivyokuwa, mke huyo wa mtu aliyetambulika kwa jina la Asha, mkazi wa Mabibo alisema alipata mawasiliano ya mganga huyo kwenye kipeperushi ambacho kilieleza kuwa, anatibu magonjwa mengi ikiwemo kuwasaidia wanawake wenye tatizo la kupata watoto.

Mama huyo alieleza kwamba, kwa kuwa ana uhitaji wa mtoto alimtafuta mganga huyo na alipompata alikwenda kwake maeneo ya Kigogo akiwa na mumewe ambapo aliambiwa ili atibiwe atoe shilingi elfu 70.

Kutokana na kwamba hawakuwa na uwezo na fedha hizo, walimuomba akashusha mpaka elfu 50 ambapo alianza matibabu na siku zilizofuata mganga huyo akawa anampigia simu na kumwambia anataka ampelekee dawa nyumbani kwake. “Mganga alikuwa anakuja ninapoishi na mume wangu maana muda mwingi anakuwa kazini, akishakuja ananichanja sehemu za siri huku akinipaka dawa kwa vidole na kunichezeachezea.

“Kuna siku aliniambia nigeuke nyuma akanipaka mafuta sehemu za siri nikiwa mtupu, naye kumbe alikuwa amevua nguo, akaanza kunishika ili aniingizie dawa, nikakataa, nikamwambia siwezi kufanya mchezo huo. “Hakuishia hapo akanipakata akaniambia ili nipate mtoto lazima aingize dawa kwa kutumia njia ya kufanya mapenzi, nikakataa. Nikamwambia aniachie hiyo dawa mume wangu aje kuniwekea, lakini alikataa akasema ni lazima aanze yeye ndiyo mume wangu afuate.

“Tulikurupushana weee, mwisho akanipa dawa ya kunawa sehemu za siri na kuniambia atakuja kuniletea dawa nyingine siku nyingine. “Matukio yote nilikuwa namweleza mume wangu, kwa hiyo Jumatano iliyopita alinipigia simu na kuniambia nimwambie mume wangu aandae elfu 12 atakuja nyumbani Alhamisi kwa ajili ya kunipa dawa ya kufunga kiunoni.

“Mume wangu aliweka mtego, mganga akaja, akaingia chumbani, akaniomba kanga nikampa akaichana kipande akafunga dawa, ile amenikumbatia ili anifunge ndiyo akanaswa na mume wangu aliyekuwa ameongozana na Polisi wa Kituo cha Mabibo,” alisema Asha. Mganga huyo alikamatwa na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Mabibo na kufunguliwa jalada la kesi lenye namba Rb Mmb\720\2018 SHAMBULIO LA AIBU!

baadaye sangoma huyo alihamishiwa kwenye Kituo cha Polisi cha Urafiki kwa hatua zaidi za kisheria. Mwandishi wetu alifanya jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP Jumanne Murilo ili kujua kama ana taarifa za kutiwa mbaroni kwa sangoma huyo, lakini hakupatikana mara moja.

Hata hivyo, mkasa huu iwe ni fundisho kwa wanawake wanaohangaikia kupata ujauzito kwani wapo waganga wengi wa kienyeji ambao ni matapeli wanaodai kutoa dawa za kunasa mimba lakini kumbe ni waongo. Ili kumsikia mke huyo akisimulia tukio zima lilivyokuwa, ingia YouTube na ufungue Global TV Online.

STORI: Gladness Mallya, Risasi Jumamosi

Comments are closed.