Mkude, Chikwende Warejea Simba

Mapema tu asubuhi ya leo, Klabu ya Simba imeingia kambini, Ndege-Beach jijini Dar ikiwa na sura za wachezaji ambao hawajaonekana kikosini muda mrefu, Jonas Mkude na Perfect Chikwende.

 

Kupitia ukurasa rasmi wa Simba wameweka picha ya Mkude na kuandika; “Umemkumbuka ? Amerudi…NguvuMoja.”

 

Kwa upande wake, Chikwende hakuonekana kwa muda mrefu, jambo lililozua sintofahamu, lakini ni miongoni mwa wachezaji walioripoti kambini.
CC; @sifaelpaul.


Toa comment