The House of Favourite Newspapers

Teleza Anayewaingilia Wanawake Azua Taharuki Arusha

0

MTU mmoja ambae amepewa jina la ‘Teleza’ kutokana na jina lake halisi kutofahamika hadi sasa, amezua hofu katika mtaa wa Murieti kwenye kata ya Murieti Mkoani Arusha baada ya kuvunja madirisha ya nyumba mbalimbali na kuwabaka Wanawake anaowakuta ndani ambapo hadi sasa Wanawake waliobakwa ni 7.

 

Ummy Kuruthumu ambaye ‘teleza’ huyo aliingia ndani kwake na walipokutana uso kwa uso Teleza alimpa ishara ya kutopiga kelele lakini baadaye Mume wake alimuona na wakati wakitafuta silaha ya kupambana nae alikimbia.

 

“Mimi niliamka wa kwanza nikaingia chumba cha mtoto wakati narudi nilkakutana naye kwenye korido alifungua dirisha na kupindua loki, hakufanikiwa kufanya chochote, muonekano wake ni mfupi amevaa bukta amejifunika macho humuoni” amesema Ummy.

 

Diwani wa Kata ya Murieti Francis Mbise ameongoza kikao na Wananchi ili kujadili mikakati ya kumkamata Mtu huyo ambaye waliomuona wanasema akiwa anavamia nyumba anakua amejipaka mafuta mwili mzima.

 

Leave A Reply