The House of Favourite Newspapers

Mkude: Simba imepata dawa ya Yondani

Jonas Mkude

KAZI imeanza sasa! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kutokana na hali ya mambo ilivyo hivi sasa ndani ya Simba baada ya kuanza mazoezi yake ya kujiandaa na msimu ujao.

 

Kikosi cha Simba hivi sasa kipo nchini Afrika Kusini kikijifua kwa ajili ya msimu ujao wa ligi pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Hata hivyo, moto wa kuzifumania nyavu ambao unaonyeshwa mazoezini na mshambuliaji wa timu hiyo raia wa Brazil, Wilker Henrique da Silva mwenye miaka 23 umeanza kuwashtua wengi ambapo kiungo wa timu hiyo Jonas Mkude amesema jamaa ni hatari sana.

 

Akizungumza Championi Jumatano, Mkude amesema kuwa dawa ya mabeki wakorofi kama Kelvin Yondani imepatikana na sasa wakikutana na Yanga hawatakuwa na hofu.

Kelvin Yondani

Alisema Yondani anatakiwa ajipange kwelikweli kukabiliana naye pindi atakapokutana naye uwanjani kwani jamaa huyo ni balaa kutokana na kuwa na sifa zote anazotakiwa kuwa nazo mshambuliaji.

 

“Tunaendelea na mazoezi yetu vizuri kabisa bila ya tatizo lolote, hata hivyo msimu ujao kazi ipo, mabeki wa timu pinzani wanatakiwa wajipange kwelikweli kwani safu yetu ya ushambuliaji hivi sasa ni balaa.

 

“Ukiachana na Meddie Kagere pamoja na Bocco (John), kuna Wilker ambaye ni raia wa Brazil, kusema kweli jamaa anajua, ana sifa zote anazotakiwa kuwa nazo mshambuliaji, kwanza ana nguvu, kasi pia anajua sana kumiliki mpira.

 

“Linapokuja suala la kufunga jamaa pia anajua kufunga kwa kichwa pamoja na miguu yote miwili, kwa hiyo mabeki wajipange kwelikweli, namuonea huruma sana Yondani,” alisema Mkude.

STORI NA SWEETBERT LUKONGE, CHAMPIONI JUMATANO

HII ndio GHARAMA ya GARI la Q CHIEF ALILOKABIDHIWA na HARMONIZE

Comments are closed.