The House of Favourite Newspapers

Mkuki Moyoni Mwangu 63

0

TUKIO la mchumba wa Jamal; Vivian kuliwa na chui mbugani Serengeti walikokwenda kwa mapumziko kabla ya ndoa yao, lilimuumiza sana, wakati huo alikuwa mwanafunzi wa udaktari katika Chuo Kikuu cha Manhattan, uamuzi alioufikia ni kuachana na masomo ya udaktari na kujiunga na chuo cha wanyamapori ili akimaliza masomo aweze kuzuia matukio mengine ya aina hiyo.

Hakutaka tena uhusiano na mwanamke baada ya tukio hilo, kufanya hivyo aliamini ingekuwa ni kumsaliti mchumba wake! Akili na mawazo yake yote yakaishia kwenye masomo na baadaye kazi alipopangwa kuwa meneja wa hifadhi ya wanyama wakali ya American National Park.

Akiwa kazini jioni moja wakati giza linaingia, alimwona msichana mrembo kupindukia akikimbizwa na simba, kwa kutumia bunduki yake alimuua simba na kumpeleka msichana huyo nyumbani kwake kwa siri bila mtu yeyote kugundua baada ya msichana huyo (Catarina) kumweleza kwamba kulikuwa na watu waliokuwa wakimtafuta ili wamuue na ndiyo waliomtupa porini ili afe kwa kuliwa na wanyama wakali.

Jamal akamtunza Catarina vizuri nyumbani kwake, akimwonyesha upendo wa kila namna! Mwisho penzi likaanza kuchipuka mioyoni mwao, kila mmoja akitamani mwenzake angeziba pengo la mpenzi wake aliyekufa, lakini hakuna aliyefungua mdomo kuzungumza!

Siku moja wakiwa katika maongezi, Jamal alibubujikwa na machozi wakati akimsimulia jinsi Vivian alivyokufa, kwa huruma Catarina akamkumbatia akimbembeleza, miili yao ikahemuka na kujikuta wakianza kupeana mabusu bila kutarajia mpaka wakazidiwa kabisa.
“Twende kitandani!” ndiyo maneno ambayo Jamal alimwambia Catarina.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…

MWILI wa Catarina ulikuwa umelegea kabisa huku akihema kwa nguvu kama mtu aliyekimbia mbio ndefu, kitendo alichofanyiwa na Jamal kilikuwa kipya, tangu azaliwe hakuwahi kusisimuliwa kiasi hicho na mwanaume! Kweli hakuwa nayo bikira yake, mwanaume mwenye roho mbaya Jackson Motown alimnyang’anya bila hiari yake katika tendo ambalo wala hakulifurahia.

Siku hiyo alijisikia vizuri kwa sababu alikuwa na mwanaume aliyempenda kutoka ndani ya moyo wake na alikuwa radhi kufanya alichotakiwa kukifanya, akatamani angekuwa hajaguswa na mwanaume ili Jamal ndiyo awe mwanaume wake wa kwanza akichukua nafasi aliyotakiwa kuichukua Kevin.
“Don’t cry!” (Usilie!) Jamal alimwambia kwa sauti nyororo ya chinichini kama vile alikuwa akigunaguna tu!

“I love you Jamal I feel so good in your arms!” (Nakupenda Jamal, najisikia vizuri sana kukumbatiwa na wewe!)
“Me too! You have occluded Vivian’s gap in my heart!” (Mimi pia! Umeziba kabisa pengo la Vivian moyoni mwangu!)
“Really?” (Kweli?)
“Sure!” (Hakika!)

“Have you ever had sex?” (Umeshawahi kufanya tendo la ndoa?)
“No! If I was a girl, I would be a virgin!” (Hapana! Kama ningekuwa msichana, ningekuwa bado bikira!)
“You did nothing with Vivian?” (Hamkufanya chochote na Vivian?)

“The promise was to do it on our wedding day!” (Ahadi ilikuwa ni kufanya tendo hilo siku ya ndoa!)
“The same story with me and Kevin, but that fool ruined my plans by stealing my virginity.” (Historia ya kufanana kwa mimi na Kevin, lakini yule mpumbavu akaharibu mipango yetu kwa kuniibia bikira yangu!) aliongea Catarina akimaanisha Jackson Motown.

“Forget about the past today is our day, let’s go to bed now, it’s time to enjoy the fruit!” (Achana na mambo ya zamani mpenzi, leo ni siku yetu, twende kitandani, ni wakati wa kulifaidi tunda!)

Jamal alimshika Catarina mkono wa kuume, taratibu akimwongoza kuelekea kitandani ambako alimbeba juujuu na kumlaza, akarudi kinyumenyume hadi kwenye swichi ya kuzima taa na kupunguza taa kadhaa zilizokuwa zikiwaka ili kutengeneza mazingira ya kuvutia na kuhamasisha, akaisogelea redio yake iliyokuwa kando na kuchagua wimbo wa Celine Dion uitwao Power of Love uliopigwa katika midundo laini.

“Have you ever tested for HIV?” (Umeshawahi kupima damu yako kuona kama umeathirika au la?) Jamal aliuliza.
“Yes! I did soon after the Jackson Motown’s incidence!” (Ndiyo! Nilipima tu mara baada ya tukio la Jackson Motown!)
“What were the results?” (Majibu yalikuwaje?)
“Negative!” (Sikuwa nimeathirika!)
“Should I trust you?” (Nikuamini?)
“Just trust me!” (Niamini tu!)

Hapakuwa na muda wa mazungumzo marefu wala hotuba tena, chumba kilibaki kimya kama vile hapakuwa na watu.
***
Mpaka miezi miwili baadaye walikuwa wakiendelea kuishi maisha ya raha mustarehe, Catarina akiwa hajaliona jua, muda wote akiwa ndani! Hofu ya kuuawa bado ilimtawala, hakuwa pia na mawasiliano yoyote na wazazi wake wala kuelewa kilichokuwa kikiendelea nje ya nyumba hiyo, alimtegemea Jamal ndiye ampe taarifa lakini hakufanya hivyo.

Tatizo kubwa lililomsumbua wakati huo likawa ni kutapika kila siku asubuhi, Jamal alihisi kitu na kuamua kununua kifaa cha kupimia ujauzito kwenye mkojo, majibu yaliyowashangaza wote wawili yaliposomea Catarina alikuwa mjamzito, mimba ya miezi miwili!
“I am so happy! You are going to be the mother of my baby! What a lucky?” (Nina furaha mno! Utakuwa mama wa mtoto wangu ni bahati kiasi gani?)

“I love you Jamal, you have taken Kevin’s position in my heart, I never knew I could be this happy with you!” (Nakupenda Jamal, umechukua nafasi ya Kevin moyoni mwangu, sikuwahi kujua ningeweza kuwa na furaha kiasi hiki nikiwa na wewe!)
“Promise one thing!” (Niahidi kitu kimoja!)
“What is it baby?” (Kipi mpenzi?)

“That we are going to get married and you will never leave me!” (Kwamba tutaoana na hutaniacha!)
“I promise you with all my heart!” (Nakuahidi kwa moyo wangu wote!)
“Mwaaah!” Jamal alimpiga busu usoni.

Je, nini kitaendelea? Fuatilia kesho katika Gazeti la Championi Jumamosi.

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, INGIA NA LIKE PAGE YA FACEBOOK YA ERIC SHIGONGO===>https://www.facebook.com/shigongotz/

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA TUFOLLOW

INSTAGRAM===>https://www.instagram.com/globalpublishers/

TWITTER===>https://twitter.com/GlobalHabari

FACEBOOK===>https://www.facebook.com/GlobalPublishers

YOU TUBE===>https://www.youtube.com/user/uwazi1

Leave A Reply