The House of Favourite Newspapers

Mkuki moyoni mwangu – 95

0

JACKSON Motown anatumia vijana wake kumteka Kevin ili wampeleke mashambani huko Opa Locka, Miami, Marekani kwenda kumuua! Zoezi hilo linafanikiwa na baadaye yeye mwenyewe anaruka kwa helikopta hadi Opa Locka tayari kwa kumuua Kevin.

Kitu ambacho watekaji hawakufahamu ni uwepo wa galoni lenye tindikali kwenye buti alimofungiwa Kevin, galoni hilo ndilo lililookoa maisha yake kwani mara tu walipofungua buti ili wamtoe, Kevin aliwamwagia tindikali wote na kukimbia akiwaacha wanagalagala chini.

Mbio zake zilimfikisha nyumbani kwa mzee mmoja ambaye mbwa wake walimbwekea sana Kevin, akatokeza na bunduki kwa lengo la kumuua! Lakini mzee huyo hakufanya hivyo baada ya Kevin kumlilia, mwisho akamkaribisha ndani ili amwelezee ni nini kilichotokea na alikuwa akielekea wapi.
Je, nini kitaendelea?

SONGA NAYO…

“MY name is Thomas Edmund!”(jina langu ni Thomas Edmund!) alisema mzee huyo mwenye ndevu nyingi zilizojaa mvi.
“Yes sir!”(ndiyo mkuu!)
“I hereby promise to take care of you because Jackson Motown is a bad guy, my enemy and the law of life says; your enemy is my friend and your friends is my enemy!” (Naahidi kukutunza, kwa sababu Jackson Motown ni adui yangu, ni mtu mbaya na sheria ya maisha inasema; adui yako rafiki yangu na rafiki yako adui yangu!)
“Thank you! Thank you so much!”(Ahsante! Ahsante sana!) Kevin aliitikia akipinda kupiga magoti mbele ya mzee Thomas ambaye kwake alikuwa mwokozi.
“Don’t worship me, I am not God!” (Usinisujudie, mimi siyo Mungu!)
Machozi yalikuwa yakimbubujika Kevin, hasa alipofikiria jinsi alivyonusurika kifo mikononi mwa Jackson Motown, kila alipowaza kama kusingekuwa na galoni ya tindikali kwenye buti alikofungiwa kifo chake kilikuwa kimefika, alimshukuru Mungu, maana kifo chake kingekuwa kibaya mno.
Alipomtazama mzee Thomas Edmund baada ya kunyanyuka na kuketi kwenye kochi, taswira ya msichana aitwaye Mariana ikamwijia kichwani na wema ambao binti huyo mrembo alimfanyia hatimaye kumkaribisha nyumbani kwake, Kevin akidhani ulikuwa ni msaada bila kuelewa alikuwa akiingia mtegoni na hatimaye kujikuta mikononi mwa Jackson Motown.
“Naye anaweza kunisaliti kweli?” Alijiuliza.
“What are you thinking?”(Unawaza nini?) mzee huyo aliuliza baada ya kugundua kulikuwa na kitu kikiendelea kichwani mwa Kevin.
“Nothing!”(hakuna kitu) Kevin alijaribu kuficha lakini ukweli wa mambo ulibaki kuwa alishaanza kumhofia mzee huyo kwa sababu ya historia ya kusalitiwa na Mariana.
Kevin alimsimulia mzee Thomas kila kitu kuhusu maisha yake, sababu ya yeye kuwepo nchini Marekani kumfuatilia mchumba wake ambaye alikuwa na uhakika kabisa Jackson Motown alifahamu aliko au alihusika kumuua, kitendo cha yeye kumfuatilia nyumbani kwake Miami ndicho kilichomfanya aingie matatani.
“She is probably dead by now or Jackson Motown captured and made her a sex slave!” (Atakuwa aidha amekufa au Jackson Motown alimteka na kumfanya mtumwa wake wa ngono!)
“All I need is to know the truth!”(Ninachohitaji ni kujua ukweli!)
“You will know it!”(Utaujua!)
“How?”(Nitajuaje?)
“Hold on, be patient!”(Subiri, kuwa mvumilivu) Mzee Thomas aliongea kwa kujiamini.
Maisha yao tangu siku hiyo yaliendelea vizuri, kwa siri Kevin akimfuatilia mzee Edmund ili apate kugundua kama alikuwa na mpango wowote mbaya lakini hakugundua chochote kwani mzee huyo hata alipokuwa akiongea na simu zake hakuondoka eneo walilokuwa wamekaa, hakuonyesha jambo lolote alilokuwa akificha zaidi ya muda mwingi kumwongelea Jackson Motown vibaya.
Kevin hakuwahi kutoka nje hata mara moja sababu ya hofu, wageni walipofika kumtembelea mzee Thomas aliongea nao nje ya nyumba yake ili wasipate nafasi ya kugundua palikuwa na mtu aliyefichwa ndani ya nyumba hiyo na walipobaki wawili macho yalielekezwa kwenye luninga wakifuatilia kama kungekuwa na habari yoyote ile kumhusu Jackson Motown.
“Kevin!” mzee Thomas alimwita usiku wakiwa wamelala.
“Yes sir!”(Ndiyo mkuu!)
“Tomorrow morning I will leave for downtown Miami!”(Kesho nitaondoka kwenye mjini Miami!)
“You are going to leave me alone?” (Utaniacha peke yangu?)
“You will be okay! Nobody knows you are here!”(Hakuna anayejua uko hapa!)
“I am worried!”(Nina wasiwasi!)
“Stop worrying and be happy!”(acha kuwa na wasiwasi na uwe na furaha!)
“How long are you going to stay there?”(Utakaa huko kwa muda gani?)
“One night!” (Usiku mmoja!)
“Oh my God!” (Mungu wangu!) Kevin aliongea maneno hayo akionyesha wasiwasi wake kwani eneo aliloishi mzee Thomas lilikuwa ni katikati ya msitu kwenye mashamba, nyumba zilikuwa mbali mno na eneo hilo.
Juhudi za kumsihi mzee Thomas asiondoke hazikuzaa matunda, kwa madai kwamba alikuwa akienda jijini kufuatilia mafao yake ya kulitumikia Jeshi la Marekani kwa miaka mingi, serikali ilimlipa kiasi fulani cha fedha kila baada ya miezi sita na wakati wa kulipwa ulikuwa umewadia.
“Ok! You can go, I will be here waiting!” (Sawa! Unaweza kwenda, nitakusubiri hapa!)
***
Taarifa alizotoa Catarina kwa FBI zilipounganishwa na alizotoa Jackson Motown wakati wa mahojiano baadaye akiwa hospitali ya New York Trauma Center alikokuwa amelazwa kutibiwa majeraha ya kuungua na tindikali usoni, hasa pale alipoelezea tukio zima la kumwagiwa tindikali na Kevin ambaye baada ya hapo alikimbia kuelekea kusikojulikana, ziliwafanya FBI kuamini kabisa Kevin alikuwa hai mahali fulani na ilikuwa ni lazima atafutwe kabla hajauawa kwa mkono wa mbali wa washirika wa Jackson Motown.
Kwenye kikao chao FBI wakakubaliana kuondoka kwa helikopta mpaka Opa Locka ambako walitua mbele ya nyumba iliyopo mbele ya shamba la Jackson Motown, wakakuta helikopta yake bado iko mahali palepale, mbwa wawili mabingwa wa kupekua na kufuatilia vitu pia walishushwa.
Kazi ya kumtafuta Kevin ikaanzia ndani ya nyumba hiyo kisha kwenye gari ambalo Kevin alifungiwa ndani yake, mbwa wakanyanyuliwa juu na kunusishwa harufu iliyokuwa ndani ya buti, baada ya hapo pua zao zikaelekea ardhini wakinusa huku wakifuatilia alikopitia Kevin, askari wakiwa nyuma na silaha zao mkononi.
Safari hiyo iliwafikisha kwenye nyumba ndogo iliyoko katikati ya shamba la maua, wakasogea karibu na kuanza kugonga huku mbwa wakibweka kwa nguvu kuashiria kwamba ndani ya nyumba hiyo ndimo alimokuwa mtu waliyekuwa wakimtafuta, sekunde chache baadaye mlipuko wa ajabu ulitokea, bomu lilikuwa limelipua nyumba iliyokuwa mbele yao, wote wakalala chini kwa mshtuko mkubwa uliojitokeza.

Je, nini kitaendelea? Kevin amekufa? Mlipuko huo umetegwa na nani? Fuatilia siku ya Ijumaa katika Gazeti la Championi Ijumaa.

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, INGIA NA LIKE PAGE YA FACEBOOK YA ERIC SHIGONGO, BOFYA HAPA ===>https://www.facebook.com/shigongotz/

Leave A Reply