The House of Favourite Newspapers

Mkurugenzi Apata Ajali

0

 

MKURUGENZI wa Taasisi ya Doris Foundation, Doris Mollel, amepata ajali leo maeneo ya Mtumba Dodoma alipokuwa akitoka kwenye kikao cha shughuli zake za kikazi.

 

 

Katika ajali hiyo Doris na Dereva wake wametoka salama licha ya yeye kupata maumivu sehemu za mbavu na shingoni.

 

 

“Namshukuru Mungu kwa kunipa nafasi nyingine ya kuishi maana ilikuwa ni ajali mbaya, imetokea maeneo ya Mtumba Dodoma, niko salama ni maumivu tu shingoni na ubavumi” amesema Doris.

 

 

Mollel, aliyewahi kuwa Miss Ilala 2013 na Miss Singida 2014, na pia ndiye mwanzilishi na wa taasisi hiyo inayojihusisha na kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti).

 

 

Leave A Reply