The House of Favourite Newspapers

Messi, Ronaldo Mtegoni UEFA

0

LIGI ya Mabingwa Ulaya, hatua ya 16 bora inatarajiwa kuendelea leo Jumanne na kesho Jumatano huku mastaa wa soka, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wakiwa katika mtihani mzigo wa kuhakikisha wanazivusha timu zao kwenda hatua ya robo fainali ya michuano.

 

Messi atakuwa na mtihani mbele ya Paris Saint-Germain ambayo itakuwa pale Paris nchini Ufaransa ikiwa na mtaji wa mabao 4-1 ilioupata Camp Nou nyumbani kwa Barcelona.Shughuli yao itakuwa kesho Jumatano, ambapo Messi akiwa nahodha wa Barcelona, ataiongoza timu yake kuona wanapindua matokeo na kusonga mbele.

 

Mchezo huo wa kesho unaweza kushabihiana kidogo na ule wa mwaka 2017, Barcelona ilianzia Msimu uliopita, Juventus iliishia hatua ya 16 kama ilivyo sasa wakati ikinolewa na Maurizio Sarri. Kwa sasa kocha wao ni Andrea Pirlo ambaye ni kiungo wa zamani wa kikosi hicho.

 

Ni wakati mwingine kwa Ronaldo kuibeba timu yake hiyo kwani tangu ajiunge nayo mwaka 2018, hawajafanya vizuri katika michuano hiyo. Hatua kubwa zaidi waliyofiika ni robo fainali, ilikuwa msimu wa 2018/19.

 

Leo Jumanne pia tutashuhudia Borussia Dortmund ikipambana na Sevilla. Mechi ya amefunga mabao nane kwenye michuano hiyo na kuwa kinara, anatarajiwa kuongoza mashambulizi upande wa Dortmund.

Liverpool wenyewe wakiwa na mtaji wa mabao 2-0, kesho Jumatano watapambana na RB Leipzig utakaochezwa kwenye Uwanja wa Puskás.

 

Baada ya kutokuwa na matokeo mazuri ndani ya Premier huku ishu ya kutetea ubingwa wao ikionekana kuwa ngumu, nguvu zao wamezielekeza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo mashabiki wao wanaamini watakuwa mabingwa msimu huu.

Leave A Reply