The House of Favourite Newspapers

Mkuu Wa Majeshi Ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob Mkunda Akabidhi Magari Timu Za Jeshi

0

Dar-es-Salaam Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania, Jenerali Jacob Mkunda amekabidhi magari matatu kwa timu za jeshi ambazo ni JKT Tanzania, JKT Queens na Mashujaa FC yenye uwezo wa kubeba abiria 56 kwa wakati mmoja.

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi magari hayo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania, Jenerali Jacob Mkunda amesema wachezaji wa timu za mpira wa miguu za JKT watakiwa kuwa na upendo umoja na mshikamano na wajue kinachohitajika ni ushindi katika ushindani kwenye kulisakata kabumbu, kucheza kwa weredi wawapo uwanjani na sio kuwa na chuki zitokanazo na michezo baina yao.

“Kilichotusukuma kuongeza nguvu ili uwezo wa kuibua vipaji vingi vilivyopo pande zote na kujiendeleza ili Taifa lipate medali nyingi, fursa njema, ajira na kuitangaza nchini kimataifa.

“Gari zipo za timu zote za JKT, leo nazindua zipo tatu na moja ipo bandarini inaweza kutoka muda wowote nayo ni miongoni mwa gari za usafiri za wachezaji wa timu hizi”amesema Jenerali Mkunda.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wales Karia, amempongeza Mkuu wa Majeshi kwa kutoa magari kwa wachezaji wa timu za JKT Qeens, JKT Tanzania, Mashujaa FC.

“Hii ni sehemu ya kutimiza ndoto zangu nilipokua na vituo vya ufundi lakini kwa sasa najivunia zaidi kuanzishwa kwa vituo vya michezo vitakavyowafikia watu wengi.” amesema Karia.

Leave A Reply