The House of Favourite Newspapers

DC Kinondoni Mgeni Rasmi Wezesha Sport Bonzana

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Wezesha Sport Bonanza linalotarajia kufanyika Desemba 2, mwaka huu kwenye Viwanja vya TTCL,  Kijitonyama, Dar es Salaam.

 

Katika bonanza hilo ambalo limeandaliwa Kampuni ya True Mark na On Sport Fitness kwa lengo la kuhamasisha watu kushiriki katika kufanya mazoezi mbalimbali ya viungo kwa ajili kuwezesha  kuwa na afya bora.

 

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo mchana kwenye ofisi za kampuni hiyo mratibu wa bonanza hilo, Agnes Mgongo amesema katika bonanza hilo la aina yake wanatarajia mgeni rasmi kuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni.

 

“Maandalizi ya bonanza yanakwenda sawa tunatarajia kuwa na michezo mingi siku hiyo kwa ajili ya watu wote watakaojitokeza kushiriki kwa kuwa litakuwa ni la bure kabisa lakini washiriki wote watapa fursa ya kupima afya zao bure kabisa.”

 

“Kwa upande wa viongozi wa serikali tunarajia kuwa na wageni wengi lakini mgeni rasmi tunategemea kuwa na  Daniel Chongolo ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kinondoni na kutakuwa na wasanii wa aina mbalimbali ambao watatoa burudani ya kutosha.,” alisema Mgongo.

Comments are closed.