The House of Favourite Newspapers

Mmiliki Mabasi Ya HBS, Sabena Aliyejiua Kwa Risasi Azikwa

MMILIKI  wa kampuni mbili za mabasi za HBS Express na Sabena, Sultan Ahmed maarufu kama Chapa, aliyejiua kwa kujipiga risasi mdomoni ikatokea kisogoni amezikwa jana jioni Sikonge mkoani Tabora.

 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Wilbrod Mutafungwa, alisema tukio hilo la kujiua lilitokea jana saa 2:30 asubuhi nyumbani kwa marehemu na kwamba chanzo cha kujiua kwake huko hakijafahamika.

Kamanda Mutafungwa alisema marehemu Chapa pia alikuwa akimiliki kituo cha mafuta ya petroli wilayani Sikonge.

Chapa anakuwa mfanyabiashara wa pili nchini kujiua kwa kujipiga risasi katika kipindi cha mwaka mmoja baada ya Festo Msalia, muuza vinywaji kwa bei ya jumla mkoani Dodoma, kujiua mwezi Machi mwaka jana.

Msalia alijiua kwa kujipiga risasi kichwani baada ya kukamatwa na shehena kubwa ya viroba vya pombe mwaka jana.

Aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoani humo wakati huo, Lazaro Mambosasa, alisema marehemu aliondoka nyumbani kwake kwa kutumia gari aina ya Toyota Prado na kwenda kujipiga risasi katika eneo la Veyula, nje kidogo ya mji wa Dodoma.

Habari na

Comments are closed.