The House of Favourite Newspapers

Mo Amkabidhi Mkude Kwa Yanga

0

UNAAMBIWA huko Simba, Jonas Mkude, mambo yake yanazidi kumwendea kombo baada ya kuwepo kwa taarifa za chini kwa chini kuwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa timu hiyo, Mohamed Dewji ‘Mo’, amegomea suala la kumuongeza mkataba mpya.

 

Mkude ni miongoni mwa wachezaji wanaomaliza mkataba Simba mwishoni mwa msimu huu.

 

Hivi karibuni uongozi wa Simba, uliwatangaza baadhi ya nyota wake walioongeza mkataba mpya, ambapo walianza na Clautos Chama, kisha wakahamia kwa wazawa, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ na baadaye John Bocco na Shomari Kapombe.

 

Chanzo chetu makini kimeliambia Championi Ijumaa kuwa, kwa namna ambavyo Mkude ameendelea kuwa na matukio ya utovu wa nidhamu, uongozi wake umesita kumuongeza mkataba kiasi cha kuruhusu hata akitaka aende Yanga.

 

Mkude hajaonekana kwenye mbili za Simba dhidi ya Dodoma Jiji juzi na ile ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Kaizer Chiefs Jumamosi iliyopita, ikieleza kuwa ameomba ruhusa kutokana na matatizo binafsi.

 

Hata hivyo, duru za michezo zinadai kuwa Simba hawana mpango wa kumbakiza klabuni hapo.“Hivi unajua kama Mkude bado hajaongezewa makataba mpya, na kwa jinsi ninavyoona sina uhakika kabisa kama ataongezewa maana uongozi hadi sasa umemchunia na uko tayari hata kumuona akisaini Yanga, maana wamechoshwa na matukio yake ya utovu wa nidhamu,” kilisema chanzo hicho.

 

Championi Ijumaa lilimtafuta Mkuu wa Maudhui wa Simba, Ally Shatry ‘Bob Chico’ ili kujua juu ya taarifa za mkataba wa Mkude, ambapo alisema: “Mkude bado yupo kikosini na atakuwa safarini kuelekea Ruangwa kwenye mchezo wetu na Namungo, hivyo taarifa za wachezaji kuongeza mkataba tayari tulishazitoa.

 

Ila kuna baadhi yao bado tupo kwenye mazungumzo nao, hivyo kila atakayekuwa tayari ameongezewa mkataba nadhani tutaweka wazi ila kwa sasa kuhusu usajili naomba utambue hivyo tu.”

NA Musa Mateja, Dar es Salaam

Leave A Reply