The House of Favourite Newspapers

Mo Atenga Mamilioni ya Ubingwa CAF

0

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’, amesema kuwa ameandaa bajeti kubwa ya fedha itakayowawezesha kufi ka mbali na kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye msimu huu.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu droo ya Caf ifanyike na Simba kuanza na Plateau FC ya nchini Nigeria na mchezo wao wa kwanza utapigwa kati ya Novemba 27-29, mwaka huu, ugenini.

 

Simba katika msimu uliopita ilitolewa katika hatua ya awali ya michuano hiyo mikubwa na UD Songo ya nchini Msumbiji baada ya mchezo wa ugenini kutoa suluhu kabla ya kuja kufungwa bao 1-0 nyumbani ambalo lilifungwa na Luis Miquissone kwa njia ya faulo.

 

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana Jumapili, Mo alisema kuwa bajeti hiyo itahusisha posho za wachezaji ambazo watapewa kila wanapopata ushindi bila ya kuangalia nyumbani au ugenini huku akisisitiza zitakuwa ni nono, kikubwa wanachoangalia ni ushindi pekee.

 

“Bejeti tuliyoiweka kwenye msimu huu katika Caf ni tofauti, haihusiani na ligi kuu kabisa ambayo itatumika kwa ajili ya posho za wachezaji ambao hao ndiyo watakaopambana, nisingependa kuweka wazi kiasi cha pesa lakini niseme kuwa posho itakuwa nzuri.

 

“Nyingine itatumika katika matumizi ya timu kama vile usafi ri wa ndege, usafi ri wa ndani, hoteli nzuri na kisasa tutakazofi kia tukiwa tunakwenda kucheza ugenini.

 

“Tuna kumbukumbu mbaya ya ushiriki wetu wa Caf msimu uliopita, ni baada ya kutolewa hatua ya awali ya michuano hiyo, hivyo hatutaki kuona inatokea tena hilo.

 

“Droo ya Caf wote tumeiona. Tunaenda kuanza Nigeria na tuna faida kubwa tatu; moja tuna wachezaji wenye uzoefu mkubwa na viwango vya juu wanaoweza kuhimili presha na kutupa ushindi.

 

“Pili, tunaenda kucheza Nigeria ambako mashabiki hawaingii kabisa uwanjani, kwa hiyo ni 11 vs 11 tu, lakini tatu tukirudi nyumbani pengine tunaweza kuwa na mashabiki nusu ya uwanja hivyo tutakuwa na faida kuliko wao,” alisema Mo.

 

UBINGWA LIGI KUU

“Tunataka kuutetea ubingwa wetu wa ligi kwenye msimu huu baada ya kuuchukua kwa misimu mitatu mfululizo, tunafahamu ligi ni ngumu msimu huu lakini tutahakikisha tunapambana hadi hatua ya mwisho ili kuhakikisha tunaubakisha ubingwa huo.

“Hapa katikati tulikutana na changamoto kadhaa ambazo uzuri tulizishtukia kwa kuwepo baadhi ya viongozi waliokuwa wanatuhujumu ambao tulikuja kuwaondoa haraka.

 

ISHU YA CHAMA IPO HIVI

“Sisi Simba tumejipanga. Chama hajaenda popote, tumeshasaini naye mkataba na atabaki na Simba. Tumemalizana na Chama na ni mchezaji wa Simba kwa miaka miwili na nusu ijayo, ni baada ya kusaini muda mrefu mkataba wa miaka miwili. “Mimi binafsi sina shaka na Chama kuendelea kuvaa jezi ya Simba kwa vipindi vijavyo, kwa kuwa ameiheshimu klabu na kuwapa kipaumbele mashabiki wake wa Simba ambao wanampenda na yeye anawapenda.

 

KESHO KUANZA KUSHUSHA VIFAA

“Kuanzia wiki ijayo Jumanne au Jumatano tutaanza rasmi kushusha mabomu (wachezaji watakaowasajili).

 

USAJILI DIRISHA DOGO

“Mpango wa Simba ni kuongeza wachezaji watatu hadi wanne katika kipindi cha dirisha dogo la usajili na pia tutaachana na baadhi ya wachezaji wetu akiwapo kiungo Mbrazili, Gerson Fraga.

“Yeye tumepokea ripoti ya kocha ikiomba kiungo mmoja mkabaji atakayekuja kuchukua nafasi ya Fraga, ni baada ya kugundulika ana majeraha makubwa yatakayomuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu. “Usajili tulioupanga utakuwa wa siri kubwa, kwani usajili hivi sasa imekuwa ni kama vita, kwani tukiweka wazi wapinzani wetu watataka kuingilia kati kwa kutaka kutuwahi.

 

“Bado hatujaandaa bajeti ya usajili, hivi sasa tunasubiria mapendekezo ya wachezaji ambao kocha anawahitaji, lakini pia Simba haina hela ila mimi ndio natoa hela yangu.

“Katika hilo la usajili nimepanga kuja na utaratibu mpya wa usajili wa wachezaji wetu kwa kuwapa mikataba mirefu kwa kuanzia miaka minne kwenda mbele, kama wanavyofanya Ulaya.

 

“Nilishalianza hilo katika msimu uliopita kwa Luis (Miquissone) ambaye nilimpa mkataba wa miaka minne ili kuepukana na kama hili lililotokea kwa Chama, mchezaji akiwa na mkataba mfupi.

 

“Usajili huo wa mkataba mrefu utazingatia kwanza suala la umri, ni lazima tumsajili mchezaji mwenye umri mdogo mwenye malengo ya baadaye na aliyekuwa katika kiwango bora.

 

KUMBE HAWANA MPANGO NA TONOMBE

“Suala la kumsajili kiungo Mukoko ni propaganda tu na wala hatujazungumzia hili suala kwenye kikao chetu cha bodi tulichokaa jana (juzi).

ipo katika hatua ya mwisho ya kukamilisha akademi yetu na kikubwa tulichopanga ni kumleta kocha Mzungu atakayesaidiana na makocha wazawa hapa nchini. Academi hiyo itawahusisha wachezaji wenye umri kuanzia miaka 12 watakaosomeshwa na klabu.

 

HANS POPE APIGWA ‘STOP’

“Kuhusu maneno ya Hans Pope tuachane nayo ila kuanzia sasa memba wowote wa bodi ya Simba hataruhusiwa kuongea na press bila idhini ya Mwenyekiti.”

Hans Pope, baada ya mechi dhidi ya Yanga iliyomalizika kwa sare ya 1-1, alisema kuna baadhi ya wachezaji wa Simba ambao anafahamu wanaihujumu timu yao, akatolea mfano wa Clatous Chama, Luis Miquissone na Larry Bwalya.

WILBERT MOLANDI NA IBRAHIM MUSSA, Dar es Salaam

 

Leave A Reply