The House of Favourite Newspapers

Mo Atuma Ujumbe Mzito Wachezaji Simba

0
Mohamed Dewji ‘Mo’.

PRESHA imezidi kupanda kila siku mpaka leo ambapo Simba itaikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, huko nyuma ya pazia Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’ ametuma ujumbe kwa
mastaa wake.

 

Simba ina mastaa kibao ambao wamekuwa wakipambana kuhakikisha timu hiyo inatetea ubingwa wao wa ligi kuu kama Meddie Kagere, Francis Kahata, Miraj Athuman, Pascal Wawa na wengine kibao.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema kuwa wachezaji wote wanatambua majukumu ambayo wamepewa uwanjani pamoja na ujumbe kutoka kwa Mo Dewji kwa kuhakikisha wanashinda mechi zote ikiwemo ya leo dhidi ya Yanga.

 

“Wachezaji wanatambua ujumbe ambao Mo amewaambia, ujumbe wake siku zote ni ushindi kwenye mechi zetu zote, kwa sasa klabu ya Simba ni kubwa kitaifa na kimataifa, kwa uwekezaji ambao tumefanya itakuwa aibu kupoteza kizembe jambo ambalo halipendezi kwa mashabiki na uongozi pia hasa linapokuja suala la mechi yetu dhidi ya Yanga.

“Uwe-kezaji ambao tumeufanya tunahitaji uwe na matokeo, hawa akina Kagere (Meddie), Shiboub (Sharaf), Bocco (John) wanatambua kazi yao, hivyo mashabiki niwaombe kujitokeza kwa wingi kuona namna itakavyokuwa, nitaongea mengi baada ya dakika tisini,” alisema Manara.

 

Msimu huu kwenye ligi kuu, Simba imecheza jumla ya mechi 13 ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 34 wapinzani wao Yanga wapo nafasi ya tatu wakiwa na pointi 24 wamechea jumla ya mechi 11.

Stori na Lunyamadzo Mlyuka, Dar es Salaam

Leave A Reply