The House of Favourite Newspapers

Yanga: Yatamba Kumepata Dawa ya Kagere

0

 

Juma Abdul.

BEKI wa kulia wa Yanga, Juma Abdul amesisitiza kuwa tayari ameshapata dawa ya kumzuia mshambuliaji hatari wa Simba, Meddie Kagere huku akiwataka mashabiki wa timu hiyo ya Msimbazi kutokwenda na matokeo kwani watarejea nyumbani wanalia.

 

Leo Jumamosi saa 11 jioni Simba na Yanga zitapambana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar katika mchezo unaotarajiwa kuwa mkali kutokana na timu zote kufanya maandalizi makali. Kagere ndiye mchezaji anayeonekana kuwatikisa Yanga kwani ndiye aliyefunga bao pekee wakati Simba ikishinda bao 1-0 dhidi ya Yanga msimu uliopita.

Mpaka sasa kwenye ligi kuu, Kagere anaongoza akiwa na mabao tisa na asisti mbili. Akizungumza na Championi Jumamosi, Juma Abdul aliyecheza mechi saba kati ya 11 ambazo Yanga wamecheza msimu huu, alisema kuwa kikosi chao kimejiandaa vikali kupambana na washambuliaji wakali leo.

 

“Tumefundishwa mbinu nyingi na mechi ambazo tumecheza zimetuongezea hali ya kujiamini, tupo sawa na tutapambana kufanya kazi ya kweli uwanjani, ni jeshi la kazi litakalozuia mipango hasa ukizingatia ligi ina ushindani.

 

“Kikubwa ambacho kinatupa nguvu ya kujiamini ni maandalizi pamoja na mashabiki hivyo tunaamini kazi yetu itakuwa kwa vitendo ndani ya uwanja, tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti.

 

“Kuhusu mchezo wa kesho (leo) ni kwamba tunaiheshimu Simba na tunawaomba mashabiki wao wasije na matokeo uwanjani kwani tumejiandaa vya kutosha kuhakikisha tunapata ushindi. Pointi tatu lazima zije kwetu Wanayanga,” alisema Abdul ambaye ni nahodha msaidizi wa Yanga.

Waandishi Wetu, Dar es Salaam

Leave A Reply