The House of Favourite Newspapers

Morrison Apanda Mpira Mazoezi Simba Mo Simba Arena -Video

0

TIMU ya Simba Agosti 17, 2020 wameanza rasmi mazoezi yanayofanyika kwenye Uwanja wao wa Mo Simba Arena uliopo Bunju nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam huku winga wao mpya Bernard Morrison akiwa kivutio mazoezini hapo.

Simba watafungua dimba la Ligi Kuu Bara Septemba 6, 2020  wakiwa ugenini Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya dhidi ya Ihefu FC iliyopanda daraja msimu huu.

Morrison amekuwa gumzo kwneye mazoezi hayo kwa mashabiki wanaoshuhudia mazoezi yao ambao wamesikika wakizungumzia kiwango chake na uwezpo wake ndani ya Simba.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilimpa ushindi Morrison kuwa anaruhusiwa kusajiliwa na timu yoyote baada ya kubaini kwamba mkataba wake una mapungufu huku tayari Simba ikiwa imemtangaza kumsajili kwa mkataba wa miaka miwili.

Hata kamati hiyo ilimpeleka Morrison kwenye Kamati ya Maadili kwa kosa la kusaini mkataba Simba wakati shauri la kesi yake halijamalizika.

Wachezaji wengine wapya waliosajiliwa msimu huu waliofika mazoezini ni Joash Onyango, Charles Ilanfya, Chris Mugalu, Ibrahim Ame, Larry Bwalya na David Kameta ‘Duchu’.

Wachezaji wa zamani waliokuwepo ni Aishi Manula, Beno Kakolanya, Ally Salim, Gadiel Michael, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Kennedy Juma, Erasto Nyoni, Hassan Dilunga, Jonas Mkude, Said Ndemla, John Bocco, Ibrahim Ajibu, Gerson Fraga, Mzamiru Yassin na Miraj Athuman.

Leave A Reply