The House of Favourite Newspapers

Morrison apata mbabe wake

0

BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji wa Simba, ambaye alisajiliwa kwa dili la miaka miwili baada ya kumalizana na Yanga, amepata mbabe wake ambaye amejibu mapigo na kumpoteza kwa rekodi.

 

 

Simba ilivutiwa na uwezo wa Morrison ambaye alianza kuuonesha akiwa Yanga ikiwa ni pamoja na kupanda mpira awapo uwanjani alipocheza dhidi ya Prisons kwenye Kombe la Shirikisho la Azam wakati Yanga ikishinda 2-0, Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

 

Kwenye mchezo huo, Morrison alifunga bao moja. Akiwa ndani ya Simba, Morrison ameendeleza makeke yake ya kuupanda mpira ambapo alifanya hivyo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United, Uwanja wa Mkapa. Simba ilishinda 4-0.

 

 

Katika mchezo huo, Morrison aliishia kupanda mpira na hakutoa pasi ya bao wala kufunga. Rekodi yake kwa msimu wa 2020/21 imejibiwa kibabe na mzawa Abdulrahman Mussa ambaye alikuwa nyota wa mchezo wakati timu yake ya Ruvu Shooting ikishinda mabao 3-0 dhidi ya Mbeya City, Ijumaa iliyopita.

 

 

Mussa alifunga bao moja na kutoa pasi mbili za mabao akimpa Fully Zully Maganga na William Patrick na kuipoteza rekodi ya Morrison ambaye akiwa Simba aliishia kuupanda mpira bila kutoa pasi ya bao wala kufunga. Jumla, Mussa amefunga bao moja na kutoa pasi tatu za mabao huku timu yake ikiwa imefunga mabao 11 na kukusanya pointi 19 ndani ya Ligi Kuu Bara.

 

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

Leave A Reply