Morrison Atuma Salamu Ligi Kuu

KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison, amefunguka kuwa licha ya hali ngumu wanayokutana nayo mwanzoni mwa msimu huu, bado kikosi hicho kina nafasi kubwa ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.


Simba, Jumatano iliyopita wakiwa
katika Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namungo, na kufikisha pointi 11 katika nafasi ya pili nyuma ya Yanga wenye pointi 15, michezo sawa.


Akizungumza na
Championi Ijumaa, Morrison alisema: “Ni kweli hatujawa na matokeo mazuri katika michezo yetu
iliyopita msimu huu kulinganisha
na wapinzani wetu, lakini niwahakikishie kuwa bado tuna muda wa kubadilisha hili na kama wachezaji tunafanya kila jitihada kuhakikisha tunapambana kutetea kombe letu msimu huu licha ya upinzani mkubwa ambao tunatarajia kukutana nao kutoka kwa wapinzani wetu.”

JOEL THOMAS, Dar es Salaam2181
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment