The House of Favourite Newspapers

Morrison, Chikwende Wapewa Silaha Kuivuruga Yanga

0

KATIKA kuonyesha kuwa amepania kupata zaidi ya matokeo katika mchezo wa Dabi ya Kariakoo utakaopigwa kesho Ijumaa, Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes ameonekana kuwaandaa nyota wa kikosi hicho, hasa Bernard Morrison na Perfect Chikwende kutandaza pira biriani.

Katika zoezi hilo, Gomes alianza kwa kuwagawa wachezaji wako katika makundi ya wachezaji watatu ambao walitengeneza umbo la pembe tatu na kucheza pasi fupifupi ‘Pira Biriani’ kabla ya kuwagawa katika makundi timu mbili za wachezaji wanne kila upande.

Timu moja ilikuwa na Taddeo Lwanga, Perfect Chikwende, Kennedy Juma na Francis Kahata huku timu ya pili ikiwa na Bernard Morrison, Chris Mugalu, Gadiel Michael na David Kameta ‘Duchu’.

 

Kati ya timu hizo mbili, Gomes alionekana kuwafuatilia kwa ukaribu zaidi Morrison na Chikwende hali ambayo inaonyesha wazi kuna jambo anataka walifanye katika mchezo dhidi ya Yanga Jumamosi.

STORI: MUSA MATEJA NA JOEL THOMAS, Dar es Salaam

Leave A Reply