The House of Favourite Newspapers

Morrison, Mugalu Wampasua Kichwa Sven

0

KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck ameweka wazi kwamba ana wakati mgumu wa kuwapanga wachezaji wake katika nafasi ya ushambuliaji kutokana na kuwa wengi huku wote wakiwa na uwezo mkubwa.

 

Sven raia wa Ubelgiji, ameongeza kuwa ujio wa wachezaji wapya akiwemo Chriss Mugalu na Bernard Morrison, kumezidi kumpa wakati mgumu zaidi.Safu ya ushambuliaji ya Simba kwa msimu ujao itakuwa na Mugalu, Morrison, Meddie Kagere, John Bocco na Charles Ilanfya.

Kocha huyo ameliambia Spoti Xtra: “Nina mastraika wanne kwa sasa ambao wote ni wazoefu, mechi moja inataka wawili, hiyo ina maana wawili watakaa benchi lakini pia wanaweza wasiwepo kabisa kwa sababu kuna wachezaji wa nafasi nyingine nao wanataka kucheza.

“Kila mmoja anaonyesha uwezo wake kwenye mazoezi kulishawishi benchi la ufundi ya kupata nafasi ya kucheza, hili ni jambo zuri kwa kocha kwa sababu nina nafasi kubwa ya kuchagua na kujaribu mifumo mingi zaidi katika kikosi changu.

Stori: SAID ALLY, Dar es Salaam

Leave A Reply