The House of Favourite Newspapers

Jeff Bezos Awa Tajiri wa Kwanza Duniani Kufikisha USD Bil 200

0

MKURUGENZI wa Kampuni ya Amazon, Jeff Bezos,  amekuwa mtu kwa kwanza duniani kuwa na utajiri wa Dola milioni 200.

Imeelezwa kuwa, hivi sasa Bezos (56) ana utajiri wa Dola za Marekani bilioni 204.6, huku akiwa amemuacha anayemfuatia kwa karibia dola Billioni 90, Bill Gates anayeshika nafasi ya pili akiwa na utajiri wa Dola bilioni 116.1.

Kwa mujibu wa Jarida la Forbes, Januari 1, 2020, Bezos alikadiriwa kuwa na utajiri wa Dola 115. Hata hivyo, kutokana na bidhaa za Amazon kuongezeka kwa takriban 80% tangu mwanzo wa mwaka,  utajiri wake umezidi kupanda.

Utajiri wa Bezos unakadiriwa kuwa ungekuwa mkubwa zaidi ya huo iwapo  asingeachana na mke wake, MacKenzie Scott, mwaka jana na kukubali kumpatia 25% ya sehemu ya kampuni hiyo.

Leave A Reply