The House of Favourite Newspapers

Motisun yazindua Kiboko Imara yenye ubora zaidi

0

kiboko (1)

Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Motisun Group Subhash Patel (wapili kushoto) akiwasha mshumaa pamoja na wawakilishi wa makampuni tanzu za Motisun Group kuashiria uzinduzi wa mabati ya Kiboko Imara. Hafla ya uzinduzi ulifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar-es-Salaam.

kiboko (2)

Balozi wa mabati ya Kiboko Jacob Steven ‘JB’ akicheza ngoma ya asili na kikundi cha KP traditional dance katika uzinduzi wa mabati ya Kiboko Imara yanayotengenezwa na kampuni ya MMI STEEL. Hafla ya uzinduzi ulifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar-es-Salaam.

kiboko (3)

kiboko (4)Mwenyekiti na mkurugenzi mtendaji wa Motisun Group Subhash Patel akimvalisha taji balozi wa mabati ya Kiboko Imara Jacob Steven ‘JB’ katika uzinduzi wa mabati ya Kiboko yanayotengenezwa na kampuni ya MMI STEEL. Hafla ya uzinduzi ulifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar-es-Salaam.

Kampuni inayozalisha vifaa vya ujenzi, iitwayo Motisun imezindua teknolojia itakayoongeza ubora na kuimarisha vifaa kama mabati kwa ajili ya kuezekea paa za nyumba na majengo.

Teknolijia hiyo ilizinduliwa jijini Dar es Salaam katika Hotel ya Sea Cliff na kutangazwa kuanza kwa shughuli ya uuzaji wa mabati hayo katika maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi.

Mwenyekiti na Muasisi wa kampuni ya Motisun, Subhash Patel alisema, teknolojia hii inahusu utumiaji wa madini ya aluminiamu na zinki ambayo huongeza ubora na kuyafanya mabati kudumu zaidi.

Alisema bidhaa hii mpya itakuwa ikipatikana chini ya kampuni tanzu ya Motisun iitwayo MMI. Bidhaa zitakuwa zikiuzwa katika maduka ya rejareja hususani katika maeneo ambapo wateja hupendelea bidhaa za ubora wa hali ya juu.

“Bidhaa hii itakuwa inajulikana sokoni kwa jina la Kiboko Imara. Ili kuiunganisha na walaji, Kiboko Imara itakuwa ikitangazwa na Msanii maarufu Jakobo Stephen ambaye anafanya zivuri katika fani yake na kuwa na mvuto kwa wengi,” alisema.

Bwana Patel anasema kuzinduliwa kwa bidhaa mpya kunaashiria juhudi za kampuni ya MMI kuongeza wigo wa bidhaa kwa kuzingatia mahitaji ya teknolojia ambayo ina manufaa mengi katika sekta ya ujenzi.

Kampuni ya MMI ni maarufu kwa uzalishaji wa bidhaa za ujenzi kama nondo ambazo zimekuwa zikiuzwa ndani na hata nchi jirani za Msumbiji, Zambia na Uganda zikiambatana na ubora.

“Tumejiandaa kikamilifu kuifanyia mauzo bidhaa hii mpya katika masoko hapa nchini na nchi   jirani ambapo pia kuna fursa ya masoko,” alisema bwana Patel.

Bidhaa za mabati zilizopakwa madini ya aluminiam na zinki zimekuwa zikikubalika sana katika masoko mengi duniani kwa ajili ya makazi ya kuishi na majumba makubwa ya biashara ambayo huweka msisitizo katika viwango vya ujenzi.

Alisema tayari kuna wimbi kubwa la asili la watu kuhamia katika matumizi ya mabati yaliyopakwa madini ya aluminiamu na zinki kutokana na kuwa na uwezo wa kudumu kwa muda mrefu.

“Ni kwa sababu hii MMI imechagua kuzalisha bidhaa hii muhimu nchini Tanzania kwa matumizi ya makazi ama miradi ya biashara,” alisema bwana Patel.

Bidhaa hii ya Kiboko Imara inatoa wigo mpana kwa matumizi mbalimbali mfano urefu, rangi na hata unene wa mabati.

 “Hii inamaanisha mapaa mbalimbali huhitaji unene na urefu tofauti wa mabati, mfano nyumba ya kuishi inahitaji mabati yenye unene wa kawaida wakati paa za majengo ya viwanda na biadhara kubwa kubwa huhitaji mabati manene zaidi,” alisema.

Kwa mujibu wa bwana Patel, utengenezaji wa bidhaa hii mpya umezingatia viwango vya kitaifa na kimataifa kwani zimejaribiwa ili kukidhi viwango vya ubora.

Leave A Reply