The House of Favourite Newspapers

Moto wa Ajabu Waibuka Kwenye Ibada ya Mazishi ya TB Joshua

0

MOTO umezuka na kuzua taharuki kwa waumini na waombolezaji katika Kanisa Kuu la Kikristo la Mataifa la mhubiri wa kimataifa, Temitope Balogun Joshua maarufu TB Joshua lililopo Lagos, Nigeria wakati zaidi ya watu 6,000 walipokusanyika katika ibada ya kuuaga mwili wa mchungaji huyo aliyefariki dunia Juni 5.

 

 

Mjane wa marehemu, Evelyn Joshua aliongoza waombolezaji wapatao 6,000 katika maandamano ya taa ili kuashiria mwanzo wa ibada ya mazishi ya mhubiri huyo wa Nigeria aliyefariki dunia Juni 5, 2021 siku chache kabla ya kusherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.

 

Wakati shughuli ya kuaga mwili ikiendelea jijini Lagos, moto ulizuka katika majengo ya kanisa hilo majira ya saa 11 jioni huku waombolezaji hao wakikimbia kuokoa maisha yao.

 

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa kanisa hilo inaeleza kuwa moto ulisababishwa na cheche ya umeme na kwamba tukio hilo lilidhibitiwa haraka na hakuna aliyejeruhiwa.

 

“Tunamshukuru Mungu kwa kuendelea kutulinda, tunawahakikishia umma kwa ujumla kuwa hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi na huduma za kusherehekea maisha ya Nabii TB Joshua zitaendelea kama ilivyopangwa,” ilieleza taarifa hiyo.

 

TB Joshua aliyekuwa kiongozi mwenye ushawishi mkubwa alifariki akiwa na umri wa miaka 57 na anatarajiwa kuzikwa Ijumaa, Julai 9, 2021 katika eneo la kanisa huko Lagos, Nigeria.

Leave A Reply