The House of Favourite Newspapers

Simanzi Mazishi ya Eng. Mfugale

0

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amewaongoza Viongozi mbalimbali na Waombolezaji kutoa salamu za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Eng. Patrick Aron Lipilima Mfugale tukio hilo limefanyika nyumbani kwa marehemu Ifunda Iringa ambapo ndipo mwili wake umepumzishwa hapo.

Baadhi ya viongozi wa Serikali akiwemo Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho, Wazir wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga, aliekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Taasisi mbalimbali, wabunge na viongozi mbalimbali.

 

Maelfu ya waombolezaji wamejitokeza kuungana na ndugu, jamaa, marafiki na viongozi mbalimbali kumsindikiza Injinia Mfugale katika safari yake ya mwisho.

 

Eng. Mfugale aliyezaliwa 1/12/1953, alifariki Juni 6, 2021 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma ameacha mke moja na watoto wanne, wa kike watatu wa kiume mmoja. Mfugale alikuwa mtoto wa pili kwa Mzee Aron Lipilima Mfugale na Bi Maria Mfugale Semgongolwa.

Eng. Mfugale amezikwa jana katika Kijiji cha Ifunda wilaya Ifunda Jimbo la Kalenga Mkoa wa Iringa na kuacha Simanzi kwa wananchi wa Ifunda na taifa kwa ujumla.

 

Wananchi wa Kijiji cha Ifunda na Watanzania wote watamkumbuka Eng. Mfugale kwa utendaji kazi yake katika sekta ya ujenzi ikiwemo ujenzi wa madaraja makubwa kama Daraja la Mfugale, Daraja la Mkapa, Kijazi Interchange Ubungo, Daraja la Kigongo (JPM) na mengine mengi pamoja na mabarabara.

Aidha Mbunge wa Jimbo hilo aneomba kujengwa Daraja la Mfugale katika Jimbo hilo. Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Cusbert Sendiga amewasihi wafanyakazi wa Tanroads kuenzi mema yake na utendaj wake.

 

 

Leave A Reply