The House of Favourite Newspapers

Moto Wateketeza Vibanda 65 vya Machinga Mwanza

0

VIBANDA zaidi ya 60 vya Wamachinga vimeteketea kwa moto mkubwa uliozuka majira ya saa 9 alfajiri leo Jumatano, Februari 12, 2020 katika soko la wafanyabiashara wadogo ‘Machinga’, eneo la Makoroboi jirani na Msikiti wa Wahindi jijini Mwanza baada ya kutokea hitilafu ya umeme.

Moto huo uliowaka kwa takribani dakika 45 ulizimwa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na wananchi, hakuna bidhaa zilizookolewa.

Mfanyabiashara Siffa Siraji amesema alikuwa anategemea biashara aliyokuwa akiifanya katika eneo hilo kuendesha maisha yake.

 

“Kipato nilichokuwa nakipata ndio nilikitumia kuitunza familia yangu. Kwa yaliyotokea sijui nitaihudumia vipi familia yangu!”

 

 

Juma Chuma amesema:  “Yaani moto huu mimi umeniacha kama yatima, yaani kwa sababu ndio ilikuwa sehemu yangu pekee ya kupatia riziki yangu.”

Naye Timoth Clemence amesema kwamba taarifa za kuzuka kwa moto huo amezipata baada ya kupigiwa simu na kusababisha apate mshtuko bila kujua la kufanya.

 

 

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Dk Philis Nyimbi,  amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amewataka wafanyabiashara kuwa watulivu wakati vyombo vya dola vinaendelea kuchunguza chanzo cha moto huo.

 

Bidhaa za wafanyabiashara wadogo 159 zimeteketea huku mabanda 65 nayo yakiteketea lakini hapakua na madhara kwa binadamu.

Leave A Reply