The House of Favourite Newspapers

MOURINHO SASA ATAKA BEKI MATATA WA KATI

Beki Harry Maguire

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho, anatakiwa kumuuza beki mmoja wa kati ili aweze kusajili majembe mengine kwenye timu hiyo.

 

Mourinho ameshasema anataka kuwa na kikosi imara kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu England, ili kuhakikisha kuwa timu hiyo inatwaa ubingwa ambao iliukosa msimu uliopita.

 

Mourinho anatakiwa kumuuza mmoja ili aweze kupata saini ya beki Harry Maguire kutoka kwenye kikosi cha Leicester City.

 

Pia Mourinho anataka kuhakikisha kabla dirisha la usajili halijafungwa anampata beki wa AC Milan, Leonardo Bonucci, ambaye anataka kumsajili pamoja na Toby Alderweireld kutoka Tottenham Hotspur ikiwa na maana kuwa atatakiwa kumuuza pia beki wake Chris Smalling

Comments are closed.