The House of Favourite Newspapers

MPOTO: RAIS NAYE NI BINADAMU ANA NYAMA, DAMU NA NYONGO

MWIMBAJI wa muziki wa mashairi ya asili nchini, Mrisho Mpoto maarufu kama Mjomba amesema kuwa vijana wengi wa Kitanzania sio wazalendo kwa sababu hawaijui nchi yao.

 

Mpoto ameyasema hayo katika mjadala kuhusu UZALENDO ulioandaliwa na kurushwa na Global TV Online leo Alhamisi, Januari 25, 2017.

 

Katika kujadili mambo ambayo yananasababisha vijana wengi kukosa uzalendo kwa nchi yao, Mpoto amesema vijana wengi wamekuwa wakibeza hata yale mema yanayofanywa na serikali chini ya Rais John Magufuli jambo ambalo linaonyesha vijana wengi wanashindwa kutambua thamani ya nchi yao.

 

“Jamani tukumbuke hata Rais naye ni binadamu, ana nyama, na nyongo, mambo anayoyafanya si ya kwake bali ni kwa manufaa ya nchi nzima, ipo siku hatokuwa Rais, atakuwa kwao Chato, lakini aliyoyafanya yatabaki kuwa ni faida kwa Watanzania wote,” alisema Mpoto.

 

Mbali na hayo, Mpoto amesema unahitajika mjadala wa Kitaifa kuhusu uzalendo ambapo amependekeza katika mjadala huo Rais Magufuli awepo na azungumze na vijana kujua wanataka nini na yeye awaeleze kama Rais ni mambo gani anayataka kutoka kwa vijana ili ushirikiano huo uinue nchi na kuijenga kwa pamoja.

FUATILIA MJADALA HUO HAPA

 

Comments are closed.