The House of Favourite Newspapers

Mr. Championi Akutana na Wasomaji Championi, Awarudishia Pesa Zao

0
Ofisa Masoko wa Global Publishers, Antony Adam (kulia) akimrudishia fedha yake msomaji wa gazeti la Championi.
Ofisa Masoko wa Global Publishers, Songolo Bilal (kushoto) akimrudishia fedha yake msomaji wa gazeti la Championi.
Ofisa Masoko wa Global Publishers, Antony Adam (kulia) akimrudishia fedha yake msomaji wa gazeti la Championi.
Ofisa Masoko wa Global Publishers, Antony Adam (kulia) akimrudishia fedha yake msomaji wa gazeti la Championi.

Gazeti namba moja Tanzania la Michezo la Championi jana kupitia Mr. Championi liliendelea kuwarudishia wasomaji fedha zao walizonunulia  gazeti hilo baada ya kukutwa wakilisoma.

 

Kila Jumamosi Mr. Championi huingia mtaani na kuwarudishia fedha zao wanaokutwa wakilisoma gazeti hilo ambapo leo Februari 22/2020 timu ya Maofisa masoko Wa Global Publishers walitembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ikiwemo maeneo ya Kariakoo na maeneo ya Ilala Boma na maeneo mengine.

 

Mr. Championi alikuwa akiwarudishia fedha wasomaji waliokutwa wakisoma gazeti la Championi ambapo pia hii ni mwendelezo wa kampuni hiyo kuendelea kuwajali wasomaji wake kupitia magazeti yake.

 

Kwa upande wao wasomaji waliokutwa na Mr. Championi na kurudishiwa fedha zao wamefurahi na kueleza kuwa wataendelea kulinunua gazeti hilo kutokana na kuwa na habari nyingi za ukweli na zenye kuvutia huku pia wakisema wataendelea kuhamasisha wengine kutolikosa gazeti hilo kutokana na kuwa na habari nzuri za michezo.

 

Wiki ijayo una nafasi ya wewe kurudishiwa fedha uliyotumia kununulia Gazeti la Championi Jumamosi linalouzwa Sh 800, kama utakutwa na Mr Championi unasoma gazeti hilo.

Leave A Reply