The House of Favourite Newspapers

Mr Eazi Aachia Albamu Yake ya Kwanza, ‘The Evil Genius’ Akiwashirikisha Mastaa Kibao

0

Staa wa Afropop, Mr Eazi ameachia albamu yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la ‘The Evil Genius’ iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu.

Video za albamu hiyo imechukuliwa katika maeneo na nchi tofauti kama, Ouidah na Cotonou, Benin; Kigali, Rwanda; Accra na Kokrobite, Ghana; Lagos, Nigeria; London; Los Angeles; na New York City.

Albamu hiyo ‘The Evil Genius’ huangazia baadhi ya kazi za kibinafsi za Mr Eazi, anapozama kwa kina katika mada kama vile mapenzi, usaliti, upweke, na familia, zinazoonyeshwa kupitia vitendo vitatu tofauti.

Washiriki katika kazi hiyo na nchi wanazotoka kwenye mabano ni Angelique Kidjo (Benin), Tekno (Nigeria), Efya (Ghana), Whoisakin (Nigeria), Joeboy (Nigeria), na washindi mara tatu wa Grammy Soweto Gospel Choir (Afrika Kusini).

Kwa upande wa watayarishaji, walikuwa pamoja na Kel-P (Nigeria), Knucks (U.K.), Michael Brun (Haiti), Andre Vibez (Nigeria), Yung Willis (Nigeria), Nonso Amadi (Nigeria/Canada), KillBeatz (Ghana), M.O.G Beatz (Ghana), E Kelly (Nigeria), Type A (Nigeria), Stikmatik (U.K.), Phantom (Nigeria), Beat Butcha (U.K.), Venna (U.K.), KDream (Nigeria) na Mr Eazi mwenyewe.

Katika kuonyesha Mr Eazi ni mwamba wa kuchanganya ladha, ndani yake yupo staa kutoka Afrika Mashariki – Kenya – Alphonce Odhiambo ‘Alpha ODH’ ambaye amemshirikisha kwenye kibao ‘Advice’.

Kwa upande wa usanifu wa jalada la albamu hiyo, Mr Eazi alishirikiana na mwanamitindo maarufu wa Nigeria, mbunifu na mpiga picha Daniel Obasi, anayejulikana kwa kazi yake nzuri alizowafanyia mastaa Beyoncé na Louis Vuitton.

Leave A Reply