The House of Favourite Newspapers

Mr. Shinda Nyumba Awa Kivutio Sabasaba

0

 

IKIWA ni maadhimisho ya Siku ya Maonyesho ya Biashara Kimataifa maarufu kama Sabasaba, Mr Shinda Nyumba ambaye ni mhamasishaji wa promosheni ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili inayoendeshwa na Global Publishers leo ameonekana kuwavutia wasomaji wa magazeti ya Kampuni hiyo ambayo ni Uwazi, Ijumaa, Risasi, Championi na Amani.

 

Banda lililopo Viwanja vya Sabasaba kinachouza vitabu vya Mtunzi Mahiri wa Hadithi na Riwaya, Afrika Mashariki na Kati ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo.

 

Katika maonyesho hayo ya 41 yanayofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere wasomaji wa magazeti hayo walionekana kuyachangamkia kuyanunua.

 

Wasomaji hao walionesha furaha yao kwa msafara huo na kuanza kuchangamkia gazeti la Ijumaa na Championi ambayo yapo mtaani kila Ijumaa kujaza kuponi kila mmoja akijaribu bahati yake kuweza kujishindia nyumba mpya na samani zake ndani hiyo na zawadi zingine ikiwemo simu za kisasa ‘smart phone’, ving’amuzi vya Ting, Dinner Set na pikipiki na zawadi kubwa ya nyumba mpya na samani zake.

 

Baadhi ya wasomaji hao walionekana kuvutiwa na muonekano wa Mr Shinda Nyumba na kuamua kupiga nae picha za Selfie kwa ajili ya kumbukumbu zao.

 

 

PICHA NA DENIS MTIMA | GLOBALM PUBLISHERS

===

VIDEO: Washindi 8 wa Droo Ndogo Shinda Nyumba Wakabidhiwa Zawadi Zao

Leave A Reply