The House of Favourite Newspapers

MR SHINDA NYUMBA ZAWADI MLANDIZI LEO

0
Mr. Shinda Nyumba akigawa vipeperushi.

 

BAHATI Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili leo itatembelea eneo la Mlandizi mkoani Pwani ambako Mr Shinda Nyumba atagawa zawadi kwa mamia ya wasomaji wa magazeti ya Global Publishers ambayo ni Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi.

 

Akizungumza na gazeti hili jana, Ofisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda, alisema lengo la msafara huo ni kuwashukuru wasomaji wa maeneo hayo kwa mshikamano wao katika kuhakikisha bahati nasibu hiyo inafanikiwa.

 

“Kama tungeweza, tungefika kila eneo kuwashukuru wasomaji wa magazeti yetu kwa sapoti kubwa ambayo wametoa katika kipindi chote hiki. Hapa tulipo tunaelekea mwishoni kabisa kwa tukio hili ambalo zawadi kubwa ya nyumba inaenda kutolewa.

Mr. Shinda Nyumba akigawa zawadi ya flat screen kwa mshindi wa droo ya nne.

 

“Tukiwa Mlandizi, tunajua hapa tutakutana na wasomaji wa Kibaha, Ruvu hadi Chalinze, kwa kutambua umuhimu wao, Mr Shinda Nyumba, yule kijana anayehisiwa kuwa ndiye mrefu kuliko wote Tanzania kwa sasa, atagawa zawadi kwa wasomaji watakaokutwa wakisoma magazeti yetu, hasa ya leo ambayo ni Ijumaa Wikienda na Championi Jumatatu, watazawadiwa hapohapo walipo,” alisema Mkanda.

 

Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya washindi wa droo ndogo ya tano kukabidhiwa zawadi zao katika tukio lililofanyika kwenye ofisi za Global Publishers zilizoko Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Washindi waliopatikana katika droo hiyo ndogo ya tano ni Geofrey Shangalawe wa Kigoma aliyejishindia seti moja ya televisheni kubwa ‘flat screen.’

NA MWANDISHI WETU, WIKIENDA

Leave A Reply