The House of Favourite Newspapers

Mrisho Ngassa: Naondoka Mbeya City

Khadija Mngwai | CHAMPIONI| Dar es Salaam

MSHAMBULIAJI wa Mbeya City, Mrisho Ngassa, amefunguka kuwa yupo mbioni kuachana na klabu yake ya sasa ya Mbeya City mara baada ya kumalizika mkataba wake mwishoni mwa msimu huu.

Ngassa alijiunga na Mbeya City katika usajili wa dirisha dogo msimu huu akitokea Fanja FC ya Oman, amesema mkataba ukiisha amepanga kuondoka kwenda Oman.

“Mkataba niliosaini hapa (Mbeya City) ni wa muda mfupi, hivyo sitarajii kuongeza mwingine. Niliondoka Fanja kwa sababu kibali changu kilikuwa na matatizo na ndiyo maana nilirudi hapa Bongo, lakini mipango yangu ikikaa sawa nitarejea kule,” alisema Ngassa.

Comments are closed.