The House of Favourite Newspapers

MSAFARA WA DIAMOND MTWARA ‘WAVAMIWA’ – VIDEO

Msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz akiwa na timu yake nzima WCB akielekea katika Tamasha la Wasafi Festival mkoani Mtwara, ghafla amejikuta akivamiwa na kundi kubwa la mashabiki wake kila walipopita njiani.

 

Diamond na timu nzima ya WCB wakiambatana na baadhi ya wasanii watakaofanya shoo kwenye Tamasha hilo, wameondoka Alhamisi, Novemba 22, 2018 na msafara wa magari nane kuelekea mkoani humo kwa ajili ya kwenda kuwapa burudani mashabiki.

 

Baadhi ya wasanii watakaotumbuiza katika Tamasha hilo ambao wameongozana na Diamond ni Harmonize, Rayvanny, Dudu Baya, Country Boy, Lava Lava, Young Killer, Navy Kenzo, Chin Bees, Mbosso, Queen Darling, mchekeshaji Dulvan na wengine kibao.

Msafara wa Diamond ‘WAVAMIWA’ , mashabiki wazuia gar!

Shoo hiyo ya Wasafi Festival inataraiwa kufanyika usiku wa Jumamosi hii, Novemba 24, katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.

PICHA NA MUSA MATEJA | GLOBAL PUBLISHERS

MOZE IYOBO “Wasafi festival Nitafia jukwaani/njooni muone”

Comments are closed.