The House of Favourite Newspapers

Msafiri Diouf Arejea kwa Kishindo Twanga

0

IMG_4480

Stori: Musa Mateja
RAPA maarufu wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Msafiri Said ‘Msafiri Diouf’ hatimaye amerejea ndani ya bendi hiyo baada ya siku chache kutimkia nchini Uingereza ambako alienda kwa ajili ya mapumziko mafupi.
Akizungumza na Toleo Maalum la Dansi, mkurugenzi msaidizi wa bendi hiyo, Omari Baraka alisema Diouf atakuwa akionekana katika majukwaa tofauti ya Twanga, japo wana mpango wa kumuandalia onesho maalum la kumkaribisha ikiwa ni njia moja wapo ya kumpongeza kufuatia kurudi huku akiwa ameachana na matumizi ya madawa ya kulevya.
“Kweli Diouf yupo Twanga baada ya kutoka Uingereza ambako alienda kwa ajili ya mapumziko, tutakuwa naye Twanga kama zamani na tumepanga kumfanyia shoo maalum ya kumkaribisha na kumpongeza kwa kuachana na madawa ya kulevya, mambo yakienda vizuri tutawatangazia siku hiyo,” alisema Baraka.

Leave A Reply