The House of Favourite Newspapers

Msaidizi wa Lowassa kuchunguzwa uraia wake

0

gari+bongo Bashi Awale anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar.KOVA111115Kamanda wa Polisi Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani).lowassa.jpg

Aliyekuwa Mgombea Urais kwa tikeki ya Chadema Edward Lowassa.

Kufuatia Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kumshikilia msaidizi wa aliyekuwa Mgombea Urais kwa tikeki ya Chadema Edward Lowassa, Bashir Fenel Awale Ally, Jeshi hilo limesema linachunguza kuhusiana na uraia wake.

Kamanda wa Polisi Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova amewaambia wandishi wa habari kwamba, jeshi hilo lilimtia mbaloni Awale mnamo 9, Novemba mwaka huu katika eneo la Mikocheni anakoishi na kumpeleka Kituo cha Polisi cha Kati, baada ya kupekuliwa alikutwa na nyaraka mbali mbali ikiwemo cheti vya kuzaliwa namba D.063711 Chenye jina la Bashir Abdi Ally kinachoonyesha alizaliwa katika hospitali ya Dodoma mnamo 11, Julai 1969.

Pia jeshi hilo lilimkuta Bashir akiwa na nyaraka zingine zikionesha anaomba uraia wa Tanzania kupitia Idara ya Uhamiaji. Bashir pia alipatikana na pasipoti nyingine inayoonesha kwamba alizaliwa, 11 Julai 1969 mjini Nairobi nchini Kenya akiwa na jina la Bashir Fenal Abdi Ally Awadhi.

Kova amesema kuwa kuna ishara kwamba mshukiwa huyo ni raia wa Kenya hivyo Jeshi hilo linaendelea kumshikilia huku likifanya uchunguzi kuhusiana na uraia wake.

Ameongezea kuwa sheria za Tanzania haziruhusu mtu asiye raia wa Tanzania kujihusisha na masuala ya kisiasa ikiwemo kushiriki katika kampeni na kupiga kura.

CHANZO: BBC SWAHILI NA THE CITIZEN 

Leave A Reply