The House of Favourite Newspapers

Msama Atekeleza Maagizo Ya Waziri Wa Ardhi

0


Dar es Salaam 30 Machi 2024: Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama ametekeleza agizo la Waziri wa Ardhi, Jerry Silaa la kwenda kuonana na Kamishina wa Ardhi Kanda ya Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema jana Machi 29, 2024 Msama amesema alienda jana ofisini kwa Kamishna wa Ardhi na kueleza kuwa kuna maelekezo amepewa atayafanya na kwa vile jambo hilo tayari lipo wizarani basi litafanyiwa kazi.

“Waziri wetu ni mtu anayefanya kazi yake vizuri sana na hakika Wizara ya Ardhi imempata mchapa kazi mzuri, nampongeza Lakini nimeona pia nitoe pia ufafanuzi zaidi kuhusu kiwanja kinachozungumziwa kilichopo Kibada wilayani Kigamboni, kiwanja hicho chenye namba DSMT 1022673 sijakivamia ni changu na nakimiliki kihalali.

“Nina nyaraka zote za umiliki, nimemilikishwa na Wizara ya Ardhi. Kuhusu kuwa na kiwanja eneo la Mbweni, hicho sikitambui na si changu,” amesema Msama.

“Nasikitishwa na diwani mmoja aliyempa taarifa zisizo sahihi Waziri Silaa kuwa nimewatapeli wananchi kiwanja na kusisitiza kuwa maneno hayo hayana ukweli na yakuchafua kwani Mimi ni mfanyabiashara wa miaka mingi anayeheshimika.

Amesema wakati mwingine madai ya kuhusishwa na viwanja yanatokana na alipokuwa na kampuni ya udalali, ambayo ilikuwa ikipewa tenda na mahakama katika masuala ya ardhi.

“Sasa kampuni inaenda kusimamia jambo fulani, kampuni inaitwa Msama watu wanajua mimi ndiye naenda kuchukua ardhi au nyumba,” amesema Msama.

Leave A Reply