The House of Favourite Newspapers

Msama Kumrudisha Rose Muhando

0
Meneja wa mwimbaji wa muziki wa Injili, Rose Muhando,  Alex Msama akiongea jambo.

 

BAADA ya mwimbaji wa muziki wa Injili, Rose Muhando kupotea kwa muda mrefu kwenye ulimwengu huo, aliyekuwa meneja wake, Alex Msama amefunguka kumrudisha kwenye chati kama zamani kwani hivi sasa amebadilika.

 

Akizungumza na Za Motomoto News, Msama alisema alimuacha Rose kwa kuwa alikuwa akiwatapeli watumishi wa Mungu fedha alizokuwa akipewa kwa ajili ya shoo na kesi kibao kujaa polisi, lakini kwa asilimia kubwa hivi sasa ame-‘change’ hivyo atamrudisha soon.

Mwimbaji wa muziki wa Injili, Rose Muhando.

“Rose alizidisha sana mambo yake ya utapeli ndiyo maana nikaacha kufanya naye kazi na tangu hapo amepotea kabisa kwenye ulimwengu wa Injili, ninamrudisha hivi karibuni tu, mashabiki wake wakae tu mkao wa kula maana ni mwimbaji mzuri sana anayejua kuimba,” alisema Msama.

STORI: GLADNESS MALLYA

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

Leave A Reply