The House of Favourite Newspapers

Msanii Jacqueline Wolper Alia Ndoa Yake na Rich Mitindo Kuvunjwa

0
Msanii Jacqueline Wolper na Rich Mitindo wakionyesha vyeti baada ya kufunga ndoa.

MTI wa ndoa ya msanii Jacqueline Wolper aliyofunga na Rich Mitindo hivi karibuni unakatwa; Ijumaa lina nyeti za ndani kabisa.

Lengo kwa mujibu wa chanzo cha karibu na Wolper ni kuhakikisha ndoa hiyo inavunjika, huku wahusika wa harakati ni wa ‘nguoni’ mwake msanii huyo.

Imeelezwa kuwa: “Kwanza walipanga kuweka pingamizi kanisani ili ndoa isifungwe ikashindikana, sasa hivi wamegeukia ufitini,” chanzo chetu kilisema.

Wolper alipotafutwa na Ijumaa kwa njia ya simu ili kuzungumzia mpango wa mahasidi kuvunja ndoa yake alijibu kwa meseji ya WhatSapp:

” Nimemuachia Mungu, nimejifunza, tumejifunza wote Mi na Mume wangu.”

Ijumaa lilipochimba juu ya fitina zinazotumiwa na wale wanaoitwa wabaya wa Wolper kutaka ndoa yake isambaratishwe lilibaini kuwepo kwa mazito yasiyoandikika.

Lakini kwa mnyambuo wa kawaida ambao Ijumaa limeunasa unahusu maisha ya zamani ya msanii huyo kabla hajaingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na Rich na baadaye kufunga naye ndoa.

Jitihada za kumpata Rich ambaye ndiye mpokea taarifa za ufitini ziligonga mwamba, lakini rafiki yake wa karibu alisema:

“Rich anaelewe hakuna ndoa inayoishi peponi, wote wamo duniani ambako kuna fitina na kuombeana mabaya.

“Yeye anachojali ni maisha, kazi zake na anafurahia kuona watoto wake wanapata malezi ya wazazi wote wawili.”

Rich na Wolper wamebahatika kupata watoto wawili hadi hivi sasa.

Chanzo kingine cha kutoka kwenye familia ya Wolper kililiambia Ijumaa kuwa baada ya kutokea kwa dhoruba iliyotishia uhai wa ndoa, wawili hao walikubaliana kujitenga na marafiki “adui” waliokuwa nao zamani.

“Maana kama mtu kakushindwa kila kona kinachofuata si sumu, basi ni kuwa nao mbali tu,” chanzo chetu kilifowadi meseji inayodaiwa kutoka kwa Wolper kwenda kwa rafiki mwingine wa msanii huyo aliyekuwa akibdilisha naye mawazo kuhusu fitina za ndoa yake.

Ndoa za mastaa na wasanii wengi Bongo zimekuwa zikivunjika mapema au kuingia katika migogoro mikubwa.

Elvan Stambuli mwandishi mwanamizi, Mhariri mahiri wa magazeti ya Udaku na burudhani kwa miaka mingi anasema:

“Chochote apandacho mtu ndicho huvuna; maisha ya urafiki wa kinafiki ni staili ya wasanii wengi hasa wa kike.

“Ukifuatilia utakuta, mwanaume mmoja akifanikiwa kuwa na mapenzi na msanii fulani basi huyo anaweza kuwazungukia wote hadi unasema si atawamaliza wote.

“Hii ni kwa nini, wasanii wengi hasa hawa wa filamu wanazungukana, wanasalitiana, wanaoneana wivu na hawapendani.

“Kwa hali hiyo hata ndoa zao lazima zitawaliwe na hizo sababu; ni jamii waliyoijenga kwa misingi ya kisaliti na kuchukuliana mabwana.

“Nawashauri wasanii na hasa wa kike ndiyo wenye shida kubwa na ndoa zao, wakitaka kutunza ndoa na uhusiano wao lazima wabadili staili ya maisha na marafiki.

“Huwezi kuwa na ndoa halafu ukabaki na marafiki walewale mliokuwa mnakesha nao ‘viwanja’ au ubaki na tabia zako zilezile; ndoa itakushinda tu.”

Usiache kutembelea Istagram ya globaltvonline kwa habari motomoto.

Stori na Rich Richard | Gazeti la Ijumaa

KUACHANA KWA HARMONIZE na KAJALA, MR PIMBI AFANYA PARTY KUSHEREHEKEA – ”HAFAI KUWA NA KAJALA”…

Leave A Reply