The House of Favourite Newspapers

Yanga Inautaka Tena Ubingwa wa Kombe la Shirikisho Kucheza Dhidi ya Kurugenzi Uwanja wa Mkapa

0
Wachezaji wa timu ya Yanga wakifanya yao.

WAKATI leo Jumapili Yanga SC itacheza mechi ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports dhidi ya Kurugenzi, uongozi wa mabingwa hao watetezi wa michuano hiyo, umetamba timu yao ipo tayari kutetea taji lao.

Yanga leo Jumapili wanatarajiwa kuwa wenyeji wa Kurugenzi inayoshiriki First League, katika mchezo wa hatua ya 64 bora utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, alisema: “Tunatarajia mchezo mgumu sana kwa kuwa huu ni mchezo wa mtoano na sio wa ligi, hivyo timu huwa zinajitoa kwa kila kitu uwanjani, lakini pia utakuwa mchezo mgumu kwa kuwa wapinzani wetu wanatufahamu kuliko ambavyo sisi tunawafahamu.

“Licha ya ugumu huo, tumekiandaa kikosi chetu kuhakikisha tunapata matokeo ya ushindi ili kuanza vizuri kampeni ya kutetea ubingwa wetu wa mashindano haya.”

STORI: JOEL THOMAS, SPOTI XTRA

KWA MARA ya KWANZA HARMONIZE na SALLAM SK WAKUTANA na KUSALIMIANA WAKIWA ZANZIBAR…

Leave A Reply