The House of Favourite Newspapers

Msanii Jay Melody Afunguka Kupata Utajili Kupitia Wimbo wake wa Nakupenda

0
Staa mwingine mkubwa kwa sasa wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania, Jay Melody

 

Jay Melody; ni staa mwingine mkubwa kwa sasa wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania ambaye anakiri kwamba, wimbo wake wa Nakupenda umempa mafanikio makubwa kipesa kwani sasa shoo hazikauki.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Jay Melody anasema kuwa, tangu mwaka huu wa 2022 uanze amekuwa na ratiba nyingi za shoo, lakini baada ya kuachia Nakupenda, ratiba zimekuwa nyingi zaidi na zaidi hivyo kumuongezea mafanikio makubwa kwenye maisha yake.

 

“Baada ya Nakupenda, niseme ukweli, shoo zimekuwa ni nyingi zaidi na zaidi. Kwa mfano Jumamosi zote nakuwa na shoo na siyo ndani tu ya Tanzania, bali hata nje ya nchi kama Kenya na sehemu nyingine nje ya Afrika. Kiukweli Nakupenda imetengeneza shoo nyingi sana,” anasema Jay Melody.

 

Wimbo huo wa Nakupenda ulitoka Julai 20, 2022, lakini hadi sasa hauna video, lakini una mamilioni ya wasikilizaji kwenye mitandao ya kusikiliza muziki.

 

STORI NA SIFAEL PAUL | GPL – GAZETI LA IJUMAA

Jay Melody_Nakupenda (Lyric video)

Leave A Reply