The House of Favourite Newspapers

ads

Msanii Peter Msechu Awekewa Puto Tumboni katika Hospitali ya Mloganzila, Dar

0

MSANII Peter Msechu amekuwa miongoni mwa watu waliopatiwa matibabu ya kuwekewa puto tumboni (intragastric balloon) katika hospitali ya Mloganzila, Dar es Salaam.

Akizungumzia matibabu hayo Januari 26,  2023 Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Mohamed Janabi amesema, matibabu hayo ya kuwekewa puto tumboni yanasaidia kupunguza uzito kwa watu wenye uzito wa zaidi ya kilo 90 ambapo Msechu ana kilo 144.

Kwa upande wake msanii huyo mbali na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha huduma za afya nchini pamoja na viongozi wote wa Serikali wanaohusika na sekta hiyo, amewaambia Watanzania wategemee mabadiliko makubwa.

“Leo ni siku ya kipekee kwanza kiafya na maendeleo binafsi kama binadamu ambaye ninahitaji afya njema baada ya kupambana muda mrefu kwa mazoezi na diet lakini mwishowe naishukuru Serikali chini ya Rais Samia kwa kutuletea huduma ya kuwekewa puto. Huduma hii inafanyika kwa uweledi mkubwa na mimi nipo rayari kupata puto langu,” amesema.

BREAKING: MWILI wa MTANZANIA ALIYEFIA VITANI URUSI WAWASILI ‘AIRPORT’ DAR, NDUGU WAANGUA VILIO…

Leave A Reply