The House of Favourite Newspapers

Msanii wa Bongo Fleva Thea Acharuka, Apiga Marufuku Kupostiwa Siku Akifariki

0
Msanii wa Bongo Muvi Salome Ndumbagwe Misayo maarufu kama Thea

SALOME Ndumbagwe Misayo almaarufu Thea; ni mwigizaji wa kitambo kunako Bongo Muvi ambaye anasema kuwa, baadhi ya watu na hasa watu maarufu wana tabia mbaya ya unafiki.

Anasema kuwa, watu hao wanapoona mtu amekufa, ndiyo wanaanza kumposti mitandaoni, lakini hawakufanya hivyo alipokuwa hai kwani hawakumu-wish hata happy birthday.

Thea anasema kuwa, ameshangazwa mno kwenye msiba wa Maunda Zorro, watu wengi walimposti, lakini akiwa hai hakuna aliyewahi kuposti hata wimbo wake au yeye mwenyewe, jambo ambalo siyo sawa hata kidogo.

Thea anadai wasanii wengi ni wanafiki

“Nasema hivi, kama mimi hukuwahi kuniposti nikiwa hai, jamani mtu asije kuniposti nikifa kwa sababu kwangu mimi naona ni unafiki uliopitiliza kabisa, sasa unaniposti mimi naona kweli? Kwa kweli sitahitaji kabisa mtu atumie picha yangu kujiandikisha maneno ya hovyo,” anasema Thea

Leave A Reply