Msanii wa Bongofleva Amtungia Wimbo Fayma, Mzazi Mwenza wa Rayvanny

Decky Real, msanii chipukizi wa Bongo Fleva

 

MSANII chipukizi wa Bongofleva, Decky Real anasema anampenda mzazi mwenza wa staa wa Bongofleva, Rayvanny, Fahyima na amemtungia wimbo wa kuelezea hisia zake.

Ameyasema hayo katika Kipindi cha¬†#Bongo255 na kuelezea kuwa mbali na kumpenda Fayma, lakini pia amekuwa shabiki mkubwa wa Rayvanny na amekuwa akimfuatilia kwa kipindi kirefu na ndiye ‘aliyem-inspire’ kuingia kwenye muziki.

 

Decky Real ambaye ni mzaliwa wa Kigoma, anasema alianza safari yake ya mapenzi mwaka 2018 ambapo hadi sasa, ametoa kazi takribani 54 ambazo nyingi bado hajaziachia mpaka sasa.

 

Amesema mpaka sasa, ameshafanikiwa kufanya kazi na wasanii kadhaa, wakiwemo Best Naso ambaye ameimba naye wimbo uitwao Nyama, Becka Fleva ambaye ameimba naye wimbo uitwao nanasi na H-Baba ambaye ameimba naye wimbo uitwao Tikiti.

 3470
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment