The House of Favourite Newspapers

MSD Yakabidhi Vifaa Vya Mil 900 Ifakara

0

SERIKALI kupitia Bohari ya Dawa (MSD), imekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya sh milioni 900 kwa Halmashauri ya Ifakara mji.

Akizungumza jana Mkoani humo Mbunge wa Kilombero Abubakar Asenga, alisema ujio wa vifaa hivyo, utasaidia kuboresha huduma za afya hivyo wanaishukuru serikali kwa hatua kubwa ya maboresho katika sekta hiyo.

Alieleza kuwa, jimbo hilo lilikuwa na kero saba muhmu na kubwa ambazo hazijawahi kutatuliwa tangu kupata Uhuru lakini Rais Dk. Samia amezitatua ikiwemo mradi wa ujenzi wa barabara, maji, ukarabati kituo cha umeme Kidatu, ujenzi wa shule za kata, vituo vya afya, zahanati na hospitali.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Dunstan Kyobya amesema ujio wa vifaa tiba hivyo ni neema kwa halmashauri hiyo.

Alisema, maboresho hayo makubwa yanayofanywa na Rais Dk. Samia ni lazima kuungwa mkono na watendaji hivyo anatoa siku 15 kuhakikisha MSD inafunga vifaa hivyo na wananchi wanaanza kupata huduma.

Leave A Reply