The House of Favourite Newspapers

Mshindi pikipiki; tuchezeni Bahati Nasibu ushindi njenje!

0

Nyumba (8)        Evans William aliyeshinda pikipiki.

Shinda Nyumba Droo Ndogo…

Mshindi pikipiki; tuchezeni Bahati Nasibu ushindi njenje!

MSHINDI wa zawadi ya pikipiki aina ya Skymark katika droo ndogo ya mwisho iliyofanyika hivi karibuni katika Uwanja wa Manzese-Bakhresa jijini Dar, Evans William amehimiza wasomaji kuendelea kushiriki bahati Nasibu ya Shinda Nyumba kwani ushindi upo njenje.

Nyumba (2)

Akizungumza na Risasi Jumamosi mara baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo juzi katika Ofisi za Global Publishers zilizopo Bamaga-Mwenge jijini Dar, Evans ambaye ni fundi magari alisema kuwa ni mfuatiliaji mzuri wa Magazeti Pendwa na Championi na alijitahidi kucheza mara kwa mara kila alipokuwa akinunua gazeti.

Nyumba (3)

“Sijui hata nielezeaje, kifupi nilichanganyikiwa kwa muda, sikuamini kabisa kama nimeshinda pikipiki, niwasihi wasomaji wenzangu tushiriki bahati nasibu hii, inalipa na kuna nyumba ambayo ndiyo zawadi kubwa ya mwisho,” alisema Evans.

Nyumba (9)

Naye Ofisa Masoko Msaidizi wa Global Publishers, David Mwaipaja alisema kuwa zimesalia wiki chache hivyo kuwaomba wasomaji wa Magazeti ya Amani, Uwazi, Championi, Risasi, Ijumaa na Ijumaa Wikienda kusoma kwa wingi na kujikatia kuponi zinazopatika katika magazeti hayo.

Nyumba (5)

“Zimesalia wiki chache kabla ya kufanyika droo kubwa ambayo itakuwa ya mwisho ambapo mshindi ataondoka na nyumba ya kisasa. Hatufanyi kwa kubahatisha, tupo katika serikali makini bahati nasibu hii inaendeshwa na watu makini chini ya bodi ya michezo ya kubahatisha.

“Siku ya ufunguzi wa bahati nasibu hii, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisimamia zoezi hili na tunatarajia na siku ya mtu kukabidhiwa nyumba pale Salasala (Dar), atakuwepo,” alisema Mwaipaja.

Nyumba (6)

Katika droo hiyo ndogo, washindi wengine walioshinda na kukabidhiwa zawadi zao ni Marian Mwakale aliyejishindia bed sheet, Richard Mauga aliyejishindia simu ya kisasa ya mkononi ‘smartphone’ pamoja na Aginita Nsemwa aliyejishindia seti ya vyombo vya ndani.

Nyumba (1)

Ndroo kubwa inatarajiwa kuchezeshwa mwezi ujao ambapo mshindi atazawadiwa nyumba ya kisasa yenye samani zake iliyopo Salasala jijini Dar.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE:@shigongotz

Leave A Reply