The House of Favourite Newspapers

Mshindi wa Bilioni 1.2 Sportpesa Apanga Kufungua Gereji Kubwa ya Kisasa

0
Florian Valerian Massawe mshindi wa bilioni 1 SportPesa

 

Florian Valerian Massawe mshindi wa JACKPOT ya SportPesa Bilioni 1,255,316,060 amesema kuwa mpango wake mkubwa kwa sasa ni kuweza kuwekeza kwenye masuala ya Garage kwa kuwa yeye ni fundi na hana mpango wa kuiacha hiyo kazi.

 

Hayo ameyasema leo alipokuwa akifanya mahojiano na kipindi cha Krosi Dongo cha Radio 255 Global Radio na aliambatana na mkewe Lightnes Massawe ambaye ni meneja wake.

Florian Valerian Massawe na mkewe.

“Nina mpango wa kuweza kufungua Garage kubwa ya kisasa ambayo itakuwa itakuwa na kila kitu kwa kuwa kwa sasa nimeajiriwa kwenye kampuni na bado ninafanya hiyo kazi.

 

 

“Kwa muda huu ninashauriana na watu wa benki kwa kuwa wao wana utaalamu kuhusu fedha na wakati huu bado hatujakaa tukikutana nao kwa mara nyingine nitawasikiliza nijue wao wanasema nini.

 

Pia ameweka wazi kuwa baada ya kutanagazwa kuwa mshindi vibaka waliweza kuvunja dirisha la nyumba yake na kuiba vifaa vyake vya kazi.

Massawe na mkewe, wakiwa ndani ya studio za +255 Global Radio wakiwa na mtangazaji Saleh Ally

 

“Baada ya kutangazwa kuwa mshindi niliweza kuibiwa kwa kuwa vibaka walivunja dirisha na kuiba PC zangu mbili ambazo nilikuwa ninazutimua kwa ajili ya kazi na wakati huo sikuwa nyumbani, (Kibaha).

“Nawashauri wale ambao wanacheza hii waendelee kwa kuwa SportPesa wapo haraka sana kwenye kutuma meseji na kupiga pale ambapo unashinda lakini wafanye na kazi kwa kuwa kama watakuwa hawafanyi kazi itakuwa ni hasara kwao.

 

“Mimi kufanya kazi hii ni sehemu ya ziada hasa baada ya kumaliza kazi zangu nimekuwa nikifanya hiyo na sina mpango wa kuacha kazi yangu,”

Leave A Reply