The House of Favourite Newspapers

Msiba wa Vaileth Bukumbi…. DC Magu “Taifa Limepoteza Mpambanaji

MWILI wa dada wa Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo, marehemu Vaileth James Bukumbi, umeagwa na kuzikwa leo Ijumaa, Juni 21, 2019, nyumbani kwao katika Kijiji cha Bupandwamhela, Buchosa – Sengerema mkoani Mwanza.

Baadhi ya waombolezaji waliotoa salam za rambirambi ni Diwani wa Kata ya Bupandwamhela, Masumbuko, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Buchosa, Mkurugenzi Kamanga Ferry Ltd, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Sengerema, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, na Mkuu wa wilaya ya Magu, Dkt Philemon Sengati.

 

Akitoa salam za rambirambi, Dkt. Sengati amesema; “Yanapotokea haya hutugusa sana, kwa sababu ni mtu tuliyempenda, tunasikitika sana kwa msiba huu, ninaamini wengi wetu tumesikitika kuondokewa na ndugu yetu huyu.

“Alikuwa ni mpambanaji kwelikweli, hawa ni akina mama wa kuigwa, huyu alikuwa ni mzalendo wa kweli mwenye nidhamu na kujituma, licha ya elimu yake ya msingi lakini alijituma na kufanikiwa kumiliki kampuni ya usafirishaji.

“Taifa limepoteza mwanamke shupavu ambaye alikuwa msitari wa mbele kuiletea nchi yake maendeleo, nNinaamini huko aliko roho yake iko sehemu salama, sisi tunapaswa kumuenzi kwa kufanya aliyoyatenda,” amesema  Dkt. Sengati.

Comments are closed.