The House of Favourite Newspapers

Video: Msigwa Atangaza Nia Ya Kugombea Urais Kupitia Chadema 2020

0

Mbunge wa Iringa Mjini kupitia CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa ametangaza rasmi nia yake ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Amesema hayo katika mkutano na wanahabari Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa ameshawasilisha taarifa rasmi kwa chama chake juu ya hatua hiyo na kuweka wazi vipaumbele vyake atakavyovisimamia endapo atapewa dhamana na Watanzania kuiongoza nchi.

 

“Kama nilivyotangaza siku chache zilizopita, leo natangaza rasmi nia yangu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa mujibu wa sheria na taratibu za CHADEMA tayari nimewasilisha taarifa rasmi ya nia yangu ya kugombea”, amesema Msigwa.

 

“Kwanini ninautaka Urais?, nataka kuongoza mageuzi makubwa ya kiutawala, kiuchumi na kielimu yatakayoleta maendeleo makubwa na ya haraka na endelevu kwa manufaa ya sasa na Tanzania ijayo”, ameongeza Msigwa.

 

Pia Msigwa amesema kuwa Bado Tanzania ni moja ya nchi masikini zaidi duniani ambapo kwa mujibu wake, uchambuzi wa Benki ya Dunia kuhusu mapato na matumizi ya kaya mwaka 2018 umeonesha zaidi ya nusu ya Watanzania wanaishi katika umasikini wa chini ya Dola 1.90 kwa mtu mmoja kwa siku.

 

Kuhusu vipaumbele atakavyovisimamia, Msigwa amesema, “endapo nitapata heshima na dhamana ya kuongoza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nitajikitia kwenye vipaumbele vikuu vitatu, kufanya mageuzi ya kielimu, kujenga utawala wa uwajibikaji na kufanya mageuzi makubwa ya kuichumi”.

 

Peter Msigwa na Tundu Lissu ndiyo viongozi wa chama hicho waliotangaza rasmi nia ya kugombea Urais mpaka sasa kwenye chama hicho na kuwasilisha taarifa rasmi kwa uongozi.

Leave A Reply